У нас вы можете посмотреть бесплатно RC MALIMA APIGA MARUFUKU UUZAJI, UNUNUAJI VIWANJA VYA WAHANGA WA MAFURIKO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
RC MALIMA APIGA MARUFUKU UUZAJI, UNUNUAJI VIWANJA VYA WAHANGA WA MAFURIKO Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, amepiga marufuku vitendo vya kuuza na kununua viwanja ambavyo Serikali imetenga kwa ajili ya kuwagawia wahangja wa mafuriko katika kijiji cha Tindiga, wilayani Kilosa, mkoani humo. Mhe. Malima ametoa agizo hilo Januari 29, 2026, wakati anagua utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, aliyoyatoa mwanzoni mwa mwezi Januari alipofika Kijiji cha Ndindiga kutoa pole kwa wananchi waliokumbwa na Mafuriko na kuagiza wananchi hao kupatiwa viwanja katika maeneo salama ili kuwaepusha na madhara ya mafuriko. Adam Malima amesema, tayari serikali imetenga maeneo mapya kwa ajili ya makazi ya wahanga hao na kusisitiza kuwa viwanja hivyo haviko kwa ajili ya kuuzwa au kununuliwa na kuwaonya vikali wananchi wanaojihusisha na vitendo hivyo na kusisitiza kuwa mtu yeyote atakayenunua kiwanja kilichotengwa kwa ajili ya wahanga wa mafuriko atakuwa amenunua mali isiyo halali. "..Atakayekuja kununua kiwanja cha wahanga atakuwa kauziwa mbuzi kwenye gunia." Amesisitiza Mhe. Adam Malima Akizungumza katika eneo hilo, Mhe. Malima ametaja wananchi waliothibitika rasmi kukumbwa na mafuriko ni wananchi 216 na ndio watakaopatiwa viwanja hivyo na kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, kuunda kamati maalum itakayofuatilia wananchi 160 waliojitokeza zaidi ili kubaini uhalali wao na kufikia muafaka utakaohakikisha haki inatendeka kwa wananchi wote. Sambamba na hilo, Mhe. Malima amebainisha kuwa Serikali itahakikisha huduma zote muhimu za kijamii zikiwemo umeme, maji safi na salama pamoja na miundombinu ya barabara zinapelekwa haraka katika makazi mapya ya wahanga hao, lengo ni kuboresha ustawi wa wananchi hao na kulinda utu wao. Mwisho