У нас вы можете посмотреть бесплатно "Niliacha Kazi Ili Kujitegemea, Nilifilisika, Haikuwa Rahisi" |SALAMA NA DANIEL KIJO PART 1 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 Kwenye maisha kuna watu ambao ukitutana nao tu unaamini wana kitu kizuri ndani yao na bila ya shaka watakua na mafanikio mengi tu huko mbele tuendako, hii ndo hisia ambayo mimi nimekua nayo toka siku ya kwanza naonana na Daniel Kijo. Mwerevu, mcheshi, ana muonekano mzuri na mkarimu, ila kubwa kabisa ana akili, mgunduzi na mtafutaji hasa, toka siku ya kwanza. Ukiachana na kwamba pengine ametoka kwenye familia ambayo kipato chake si kibaya na amesoma shule nzuri sana, Daniel hakuwahi kijikweza na kujiona yeye BORA zaidi ya wengine alionao chumba kimoja. Nilikutana nae EATV wakati yeye akiwa bado mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lakini wakati huo huo anafanya kazi ili mambo yake mengine yaende vizuri. Na kazi alikua anaifanya kwelikweli, ikiwa ya kutaarisha yani kwenda kuitafuta habari na kuifanyia uchunguzi na kuhakikisha inarekodiwa vizuri, na kama itahitaji sauti basi ataiwekea na mwisho kabisa yeye ndo atakua mtangazaji wa hiko kipindi wakati watazamaji wanakiona kwa mara ya kwanza. Nadhani utashi huo ndo ulimfanya aone unajua nini, mbona mi naweza kufanya mwenyewe hii? Mbona nisitoke tu hapa na kuanzisha kitu changu mwenyewe? Na hilo alilifanya. Daniel ananielezea mitihani aliyopitia baada ya kuamini kama anaweza kufanya shughuli za uzalishaji wa vipindi na mauzo mara baada ya kujikusanyia PENSHENI yake, anakumbuka kama wakati huo ulikua ukiacha kufanya kazi, ulikua na uwezo wa kwenda kuchukua NSSF yako na ukajianzishia biashara yako. Daniel anasema alienda akanunua ma camera na vifaa vyengine akiamini kabisa kama maisha ndo yameanza sasa, ila dunia ndo ilimuonyesha kwamba ki ukweli vitu si RAHISI kama ambayo alikua anadhania. Na kwenye kipindi hiki ndo ambacho aliwajua Ndugu zake ni nani na marafiki zake ni nani. Maana Rhumba lilikua si la NCHI hii. Daniel ameshawahi kuanzisha na kufanya vipindi mbali mbali vya TV hapa nyumbani na kwenye TV stations tofauti tofauti kwahiyo ashakutana na mabosi na wafanyakazi wa aina tofauti tofauti sana. Na akiwa huko kwenye safari yake hiyo ndo imemjenga awe huyu ambaye tunampenda na kujifunza kutoka kwake sasa. Miaka ya hivi karibuni Daniel amekua akiyafanyia kazi mashirika mbalimbali ya habari ya kimataifa hapa nyumbani na hii ni kazi ambayo yeye na MKE wake walipambana nayo sana mpaka ikadondokea kwenye mapaja yao. Daniel pia anatuhadithia jinsi ambavyo alikutana na mke wake, mazingira ambayo walikutana na jinsi ambavyo walianza kuongea, mara ya kwanza alivyompeleka kwa wazazi wake na jinsi ambavyo wanaishi kwa misingi ya kujijali wao na afya zao. Daniel anatuambia jinsi ambavyo anapenda anavyokua anaenda shuleni kwa mtoto wake na kuwa yeye ndo Baba cool kuliko wazazi wengine, na hii anaipambania sana kwasababu ni moja ya vitu vinavyompa raha. Daniel anapenda mazoezi, analinda afya ya akili yake na mwili wake na ni mtu ambaye anajifunza sana, tena kila siku. Yangu matumaini episode hii yangu na Rafiki yangu itakusaidia hapa na pale kuhusu kujiamini na kujijali ki mwili na ki roho maana mwisho wa siku, hakuna anayekuja kukusaidia kwenye hayo. Mwisho wa siku hayo ni maisha yako na jinsi gani unataka kuyaishi ki ukweli ni juu yako. Tafadhali enjoy, Love, Salama. Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One The Incredible & Msam... Follow: Twitter: / yahstonetown Instagram: / yahstonetown Facebook: / yahstonetown Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz