У нас вы можете посмотреть бесплатно KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 21/01/2026 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 21/01/2026 UJUMBE WA LEO: MAMBO YA KUOMBEA KATIKA MSIMU MPYA (Prayer Priorities for a New Season) Mhubiri 3 : 1 Ni kukufahamisha maeneo muhimu ya kuombea katika msimu wako mpya, ili uimarishwe katika mahusiano yako na Mungu na ufanikiwe kimaisha. Msimu mpya, kibiblia, una maana ya kipindi kipya, majira mapya, au nyakati mpya ambazo hujawahi kuziishi hapo awali. Msimu mpya ni majira mapya yaliyowekwa na Mungu kwa kusudi maalumu la kiungu. Mhubiri 3 : 1, 11, 17 1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 11 Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho. 17 Nikasema moyoni mwangu, Mungu atawahukumu wenye haki na wasio haki; kwa kuwa kuna wakati huko kwa kila kusudi na kwa kila kazi. Matendo 17 : 26 - 28 26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; 27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. 28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. Usiache kumwombea mtu ambaye Mungu amemtuma kukusaidia unapoingia katika msimu wako mpya. 3. OMBA MUNGU AKUPE NEEMA Neema ni nini? 1. Neema ni zawadi kutoka kwa Mungu inayokufanya ukubalike mahali ambapo huna vigezo vya kukubalika. Mwanzo 39 : 4 4 Yusufu akaona neema machoni pake, akamtumikia. Naye akamweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na yote yaliyomo akayaweka mkononi mwake. 2. Neema ni nguvu ya Mungu inayoshughulika na udhaifu. 2 Wakorintho 12 : 9 9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. 3. Neema ni nguvu ya Mungu inayokuwezesha kufanya kazi kupita wengine. 1 Wakorintho 15 : 10 10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami. 4. Neema ni kipawa cha Mungu kiletacho wokovu Mwanzo 6 : 8 8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana. FAIDA ZA KUWA NA NEEMA YA MUNGU 1. Neema ya Mungu hutajirisha. 2 Wakorintho 8 : 9 9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. Luka 4 : 18 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 2. Neema ya Mungu hushughulikia mahitaji yetu - riziki 2 Wakorintho 9 : 8 8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema; 3. Neema ya Mungu huondoa vizuizi. Zekaria 4 : 6 - 7 6 Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi. 7 Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie. Msimu mpya hauhitaji juhudi mpya tu, unahitaji neema mpya. Mhubiri: Mwl. Davidney Kaale Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com