У нас вы можете посмотреть бесплатно MBUNGE ASENGA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANG’ULA “B” NA MWAYA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MBUNGE ASENGA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANG’ULA “B” NA MWAYA Mbunge wa Jimbo la Kilombero, Abubakari Asenga, ameendelea na ziara yake ya kikazi katika Kata ya Mang’ula “B” na Kata ya Mwaya, Halmashauri ya Mji Ifakara, kwa lengo la kukagua na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa ndani ya siku 100 za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan. Katika ziara hiyo, Mbunge Asenga alikagua ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari Abubakari Asenga, mradi wenye thamani ya shilingi milioni 34, ambapo milioni 4 zimetolewa na Mfuko wa Jimbo na milioni 30 kutoka Serikali Kuu. Pia alikagua mradi wa maabara ya TEHAMA (Computer Lab) unaolenga kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa kutumia teknolojia. Akiwa Kata ya Mwaya, Mbunge huyo alikagua ujenzi wa madarasa mawili na matundu sita ya vyoo katika Shule ya Awali Kiswanya, mradi unaotarajiwa kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto wa awali. Aidha, Mbunge Asenga alipokea taarifa ya mafanikio yaliyopatikana ndani ya siku 100 katika Kata ya Mang’ula “B”, ikiwemo vikundi viwili kunufaika na mkopo wa asilimia 10 ya mapato ya halmashauri wenye thamani ya shilingi milioni 7. Kaya 113 zimenufaika na mpango wa kuondokana na umaskini pamoja na kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote, huku kaya 278 zikisajiliwa kwenye mpango wa TASAF. Kupitia kampeni ya Zero Malaria, kaya 2,881 zimesajiliwa na kupatiwa vyandarua. Katika sekta ya afya, chumba cha upasuaji katika Kituo cha Afya Mang’ula kimekamilika na kiko tayari kuanza kutoa huduma. Vilevile, mradi wa umeme katika vitongoji viwili vya Kijiji cha Kanyenja unaendelea kunufaisha wananchi. Kijiji cha Mang’ula pia kimepokea mifuko 30 ya saruji kutoka Ofisi ya Mbunge kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za maendeleo.