У нас вы можете посмотреть бесплатно WAUMINI KANISA LA MBEYA KATI WACHANGIA DAMU SALAMA KATIKA IBADA YA SHUKURANI 2025 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MBEYA Waumini wa kanisa la waadventista wa sabato Mbeya Kati wameshiriki zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiari ikiwa ni moja ya lengo la utume walilojiwekea la kuwahudumia wahitaji na wenye shida ili kuwapatia mahitaji Mratibu wa damu salama kanda ya Mbeya Bi Latifa Nyakunga akielezea lengo la kuendesha zoezi hilo mesema wameguswa kufika kanisani hapo mara baada ya kupata dharura ya upungufu wa akiba yad amu salama katika hospitali kuu ya kanda ya Mbeya Bi latifa Nyakunga ameongeza na kutoa pongezi kwa washiriki wa kanisa la waadventista wasabato kwani wamekuwa wadau wakubwa katika uchangiaji wa damu na ushirikiano uliopo baina yao na kanisa la waadventista wa sabato ndio haswa umewafanya kuendelea kuendesha mazoezi hayo kila kunapokuwa na upungufu wa damu Naye Mchungaji wa kanisa na Mtaa wa Ruanda Meshack Jackson Zilakwega amesema kama kanisa wanalo lengo la kufanya utume na kuwafikia wengi zaidi bila ya kuwasahau wale wenye uhitaji wad amu salama kwani kwa kufanya hivyo wanawaanda kumjua Kristo Mzee wa kanisa Fredy Bingibosa Pamoja na mshiriki aliyechangia damu wameeleza jinsi tendo hilo lilivowagusa na kuamua kushiriki kwa kutoa sadaka hiyo kwa wahitaji na kutoa rai kwa washiriki wengine kuendelea kujihusisha kwa utume wa matendo ya huruma kila inapohitajika kufanya hivyo Zoezi la uchangiaji wad amu katika kanisa la Mbeya kati limefanywa ikiambatana na ibada ya shukrani kwa Mungu kwa kuwalinda kwa kipindi chote cha mwaka 2025 na kumuomba Mungu kuwaimarisha zaidi kwa mwaka 2026 Na George Muttarogwa