У нас вы можете посмотреть бесплатно #TAZAMA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Bw. Omary Chingwile ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Liwale na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo. “Hatuwezi kufanya mchezo na fedha ya Serikali. Tunahitaji kila mradi uende vizuri, fedha iliyoletwa lazima itumike kama ilivyokusudiwa.” Mheshimiwa Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza matumizi mazuri ya fedha za umma ili zikamilishe miradi ya maendeleo ya wananchi na kwamba Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote anayetumia vibaya fedha za umma. Waziri Mkuu amemsimamisha kazi mtumishi huyo jana (Alhamisi Oktoba 7, 2021) wakati akizungumza na madiwani, watumishi na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Lindi. Pia, Waziri Mkuu amelitaka Balaza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale lisimamie vyema fedha za miradi zinazotolewa katika Halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato. “Waheshimiwa madiwani, Halmashauri yenu inakusanya mapato hadi asilimia 100 lakini hatujawahi kuona mradi wowote unaotekelezwa na halmashauri na ukawa wa mfano.” Alisema Halmashauri hiyo imekuwa ikiweka makadirio madogo ya makusanyo ili ionekane inakusanya kwa asilimia kubwa lakini hata mapato yanayokusanywa, hayakusanywi kwa njia za kielektroniki na kumuagiza Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Gervas Bidogo kuhakikisha vifaa vyote vya kukusanyia fedha kwa njia ya kielektroniki (POS) vinafanya kazi. Follow us on: FACEBOOK; SpotiLeo: / spotileo-176. . HabariLeo: / habarileo DailyNews: / dailynewstz INSTAGRAM; HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig... SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid... TWITTER; Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09