У нас вы можете посмотреть бесплатно MAAJABU YA NDIZI VUMBA CHWAKA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kampeni ya Usafi wa NDizi Vumba imefanyika kijiji cha Chwaka ikiongozwa na Klabu ya Afya na Mazingira (SEIC) Tawi la SUZA Chwaka Skuli ya Biashara kwa kushirikiana na viongozi wa kijiji wanafunzi wa vyuo na jumuiya mbalimbali kwa lengo la kuboresha usafi wa mazingira na kuimarisha mshikamano wa jamii. Mjumbe wa Sheha Chwaka eneo la Kaskazini ambapo ni eneo pia la Skuli ya biashara chwaka Rajab Khamis Mtumwa Silima amesema changamoto kubwa ni ukosefu wa eneo rasmi la kutupa taka hali inayowafanya washindwe kufanya usafi wa kijiji kizima. Ameeleza kuwa usafi hufanywa kwa utaratibu wa mara kwa mara na safari hii wameungana na wanafunzi wa SUZA kuongeza nguvu katika zoezi hilo. Mwenyekiti wa Klabu ya Afya na Mazingira (SEIC) Tawi la SUZA Chwaka Skuli ya Biashara Muntathir Maulid Fakih amesema kampeni hiyo imefungwa rasmi kwa muhula wa kwanza wa masomo kwa jina la Usafi wa NDizi Vumba. Ameeleza kuwa kampeni imejikita katika kufanya usafi wa pamoja na kula chakula cha asili cha Zanzibar hususan ndizi vumba na samaki ili kuimarisha upendo na ushirikiano. Ameongeza kuwa ni mara ya kwanza Chwaka kupokea idadi kubwa ya washiriki jambo linaloonesha ari ya vijana kupenda mazingira. Hata hivyo amesema uhaba wa vifaa umeathiri utekelezaji kwa kiwango kamili na kutoa wito kwa wizara na jumuiya husika kuunga mkono juhudi hizo. Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Jimbo la Chwaka Hassan Muhammed Ukusi amesema vijana wa CCM wamefurahishwa na kampeni hiyo na kuamua kuungana na wananchi katika shughuli za usafi. Amesema usafi wa pamoja hujenga furaha mshikamano na kuunga mkono juhudi za viongozi wa kitaifa. Nae Naibu Waziri wa Afya na Mazingira wa SUZASO Thani Othman amesema amefarijika kuona wanafunzi wa SUZA wakichochea mabadiliko ya kijamii kwa vitendo. Amesema SUZASO imejipanga kushirikiana na klabu na jumuiya za SUZA kulinda mazingira na kuwataka wanafunzi kuendelea kuwa mabalozi wa uhifadhi wa mazingira. Kampeni hiyo ilishirikisha wanafunzi kutoka Skuli ya Biashara Chwaka pamoja na wanafunzi wa skuli mbali mbali suza huku vyuo vingine vikiwemo Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) na Chuo cha Utumishi wa Umma na Utawala Bora (IPA) Nazo jumuiya mbalimbali zikitoa ushirikiano wao.