У нас вы можете посмотреть бесплатно TUKIO LA WANAFUNZI KUCHEZEA MBWA NUNGWI LAZUA MJADALA, WIZARA YACHUKUA HATUA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kufuatia kusambaa kwa picha zinazoonesha wanafunzi wa Zanzibar Hope School wakimchezea mbwa, tukio hilo limezua mjadala mkubwa katika jamii kutokana na kugusa mila, desturi na maadili ya Mzanzibari. Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Wizara ya Elimu Mkoa wa Mjini Magharibi, Naibu Katibu Mkuu Utawala wa Wizara ya Elimu Zanzibar, Amosi John Enock, amesema wizara inakemea kitendo hicho na tayari imeanza kuchukua hatua za kisheria na kiutawala dhidi ya tukio hilo, ikiwemo kuifuatilia kwa kina skuli husika. Aidha, ameomba radhi kwa jamii kutokana na taharuki iliyojitokeza. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA), Ndg. Khamis Juma Khamis, amesema kampuni inayohusishwa na tukio hilo imesajiliwa kisheria kwa ajili ya huduma za chanjo kwa mbwa, usafirishaji wa wanyama na malezi, huku akisisitiza kuwa usajili wake uko halali kwa mujibu wa taratibu. Naye mmiliki wa skuli hiyo, Ndg. Juma Khatib Ali, ametanguliza kuomba radhi kwa jamii na kufafanua kuwa lengo la zoezi hilo lilikuwa kuwafundisha wanafunzi namna ya kuishi na mbwa kwa ustaarabu, ili kuepuka vitendo vya kuwaonea au kuwapiga mawe wanapowaona mitaani. #ASAMOnlineTV #ElimuZanzibar #Nungwi #MaadiliYaJamii #HabariZaLeo