У нас вы можете посмотреть бесплатно BASHUNGWA: KAZI YA KUONDOA TOPE KATIKA MJI WA KATESH IFANYIKE USIKU NA MCHANA, JENISTA NAE ASEMA.. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
📍HANANG - MANYARA 🇹🇿 Waziri wa Ujenzi, Innocent. Bashungwa amewaagiza wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kushirikiana na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini ( TARURA) kwa pamoja kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ya kuondoa tope kwenye makazi ya watu na kwenye miundombinu katika mji wa katesh Wilayani Hanang. Waziri Bashungwa ameyasema hayo wakati alipoambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista J. Mhagama, Waziri wa Madini, Anton Mavunde kukagua hali ya miundombinu na kujionea jitiada za uokoazi unaoendelea, leo tarehe 4 Disemba 2023. Kwa Upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista J. Mhagama amesema kazi ya uokozi inaendelea ikiwa ni pamoja na utafutaji wa miili inayosadikika bado haijapatikana. Amesema Serikali inaendelea kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wanagharamia shughulia za mazishi, ikiwa na kutoa matibabu bure na huduma zote kwa waathirika wa maafa haya.