У нас вы можете посмотреть бесплатно " WALIMU MMEFANYA KAZI KUBWA ,TUNADENI LA KUFUTA SIFURI " DC SWEDA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, amewataka walimu kuhakikisha wanasimamia ufaulu wa wanafunzi na kuondoa kabisa matokeo ya daraja sifuri (zero) katika shule za msingi na sekondari. Ameyasema hayo Machi 18, 2026 Mhe. Sweda ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, uliolenga kufanya tathmini ya maendeleo ya elimu na kuweka mwelekeo wa kuboresha taaluma. Katika kikao hicho, Mkuu huyo wa Wilaya aliwapongeza walimu kwa juhudi wanazozifanya katika kuinua sekta ya elimu, huku akisisitiza kuwa wao ni nguzo muhimu katika mapambano dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini, kama alivyoeleza Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Aidha, Mhe. Sweda aliipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha elimu kupitia sera thabiti, ujenzi wa miundombinu ya shule, ajira za walimu, utoaji wa elimu bila malipo pamoja na ushiriki wa wazazi na walimu katika kuinua taaluma. Pia, Mkuu wa Wilaya aliwataka walimu wakuu kuwa viongozi na walezi wa walimu wengine, huku wakishirikiana katika kutekeleza majukumu ya kitaaluma ili kufikia azma ya “Njombe bila ziro inawezekana.”