У нас вы можете посмотреть бесплатно MAKUBWA YAENDELEA KUFANYWA NA MHE. PONDEZA RAMADHANI HII или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni, Mhe. Ussi Salum Pondeza amewaasa watu wenye uwezo katika jamii kujitokeza kuwasaidia wananchi hususan katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mhe. Pondeza ametoa wito huo wakati wa hafla ya iftari ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Shangani, Shehia ya Pitanazo, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Amesema mwezi wa Ramadhani ni kipindi muhimu kwa Waislamu kufanya matendo ya kheri ikiwemo kuwasaidia wahitaji ili kupata fadhila na baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni, Mhe. Makame Mohammed Sufiani amesema wataendelea kudumisha utamaduni huo wa kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha wanawafikia wananchi wengi zaidi. Nao wananchi wa Pitanazo wamewashukuru viongozi hao kwa kuandaa iftari hiyo ya pamoja, huku wakitoa wito kwa watu wengine wenye uwezo kuiga utamaduni huo wa kusaidia jamii hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Iftari hiyo iliandaliwa na Mhe. Ussi Salum Pondeza ikiwa ni sehemu ya kuendeleza utamaduni wa kufutari pamoja na wananchi wa kijiji alichozaliwa. #ASAMOnlineTV #Ramadhani #IftarYaPamoja #Chumbuni #MsaadaKwaJamii