У нас вы можете посмотреть бесплатно RC GEITA,AWAFUKUZA KWENYE KIKAO MAAFISA WATATU WA GGML или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella, amewamuru maafisa watatu wa Kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) kuondoka kwenye ukumbi wa kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) baada ya kutoridhishwa na majibu yao kuhusu malimbikizo ya pesa za Uwajibikaji wa Makampuni kwa Jamii (CSR) ambazo hazijatolewa kwa muda mrefu. Shigella alieleza kuwa fedha za CSR ni mali ya wananchi na siyo za wafanyakazi wa GGML, akisisitiza kuwa utekelezaji wa malipo hayo haupaswi kuchukuliwa kama hisani. Aliongeza kuwa fedha hizo zimetolewa kwa mujibu wa sheria na kanuni za madini, na hivyo kampuni hiyo inapaswa kuzitekeleza bila kuchelewa. Mbunge wa Jimbo la Chato, Dk. Medard Kalemani, alikubaliana na uamuzi wa Mkuu wa Mkoa na kutoa pongezi kwa hatua hiyo, akisisitiza kuwa kanuni ya 140 ya sheria za madini inazitambua fedha za CSR kama sehemu ya utekelezaji wa sheria na siyo kama sadaka. Maafisa hao hawakuwa tayari kuzungumzia msimamo rasmi wa GGML baada ya hatua zitakazochukuliwa kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Geita.