У нас вы можете посмотреть бесплатно MKUU WA WILAYA YA RUNGWE ASHUHUDIA WAHANDISI 54 WAKILA KIAPO CHA UTII или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Beno Malisa amewataka wahandisi wote wa mkoa huo kuhakikisha wanahuisha leseni zao za kihandisi kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosimamia taaluma hiyo. Kauli hiyo imetolewa mkoani Mbeya na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Jafarr Haniu aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa katika hafla ya kula kiapo kwa wahandisi mahiri 52 iliyofanyika katika ofisi za TANROADS mkoa wa Mbeya. Amesema uongozi wa mkoa hautavumilia mhandisi yeyote asiye na sifa zinazotambuliwa na Serikali, ikiwemo kuwa na leseni halali ya kufanya kazi za kihandisi, na kusisitiza umuhimu wa kuhuisha leseni kwa wakati. Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Mhandisi Erick Nestory amesema Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) imeweka kambi mkoani humo ili kuwahudumia wahandisi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa karibu zaidi. Naye Wakili Msomi kutoka ERB ameeleza kuwa kiapo cha wahandisi ni ibada inayowataka wahandisi kuzingatia weledi, uadilifu na miiko ya taaluma katika utekelezaji wa majukumu yao. Jumla ya wahandisi 54 wamekula kiapo cha utii kwa taaluma, wakiahidi kuzingatia maadili na viwango vya uhandisi katika utendaji wao.