У нас вы можете посмотреть бесплатно “Sijawahi kupewa vitu vya burebure ama vitu vya dezo kwa Kiswahili cha mjini - JPM или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Rais wa Tanzania, John Magufuli ametunikiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa leo Alhamisi Novemba 21, 2019 na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) akibainisha kuwa alipoelezwa kuhusu suala hilo alijiuliza sababu za kupewa bure bila kuisotea. “Baada ya kuambiwa kwamba nitatunukiwa shahada ya Udaktari wa Falsafa nilijiuliza maswali mengi, lakini baada ya kukumbuka kuwa mara nyingi shahada hizi za heshima hazitolewi kwa maana ya kumpa mtu binafsi bali zinakuwa kwa niaba ya watu wengine” “Sijawahi sana kupewa vitu vya burebure ama vitu vya dezo kwa Kiswahili cha mjini, nakumbuka zamani hata nikienda kuomba hela ya kalamu baba alikuwa hanipi kirahisi, alinipa kazi ya kufanya kama vile kuchunga ng’ombe ili akikupa hela na wewe uwe umeilipia” “Lakini baadaye nikasema nikubali kutunukiwa kwa heshima ya Rais Mstaafu Mkapa (Mkuu wa UDOM) na sababu ya pili niliona kuwa shahada hii ya heshima niliyopewa ni heshima si tu kwangu bali kwa wote waliowezesha mafanikio tuliyofikia kwa miaka hii minne” “Shahada hii kimsingi imetolewa kutokana na mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano, mafanikio hayo hayatokani na juhudi zangu binafsi bali kwa ushirikiano wa Watanzania wote” “Tunaendelea na ujenzi wa reli ya kisasa takribani kilomita 700 kutoka Dar es Salaam hadi Makutopora kwa gharama ya Tsh. tril. 7.062, upanuzi wa viwanja vya ndege 11, pia upanuzi wa bandari zetu kubwa tatu za Dar, Mtwara na Tanga kwa gharama ya Tsh tril. 1.2” “Miradi ya REA, wakati tunaingia madarakani ni vijiji 2,118 ndivyo vilikuwa na umeme, sasa ni vijiji zaidi ya 8,000 vimeshapelekewa umeme” “Kutokana na juhudi zetu, tumeendelea kupata mafanikio, uchumi wa nchi yetu unaendelea kuimarika ambapo kwa sasa unakua kwa wastani wa 7% na kuifanya nchi yetu kuwa miongoni mwa nchi tano ambazo uchumi wake unakua kwa kasi barani Afrika” Amesema baba yake alikuwa hampi kirahisi vitu alivyokuwa akiomba na kutoa mfano kuwa akiomba kalamu alimpa kazi ya kufanya kabla ya kumpatia. Rais Magufuli amesema wahitimu wote 6,488 hakuna alipewa bure bali wote walisotea na kwamba bure haina heshima, ni kunyimwa kujidai na inatesa.