У нас вы можете посмотреть бесплатно Walininywesha Sumu, Nilitaka Kujiuzulu...Magufuli asimulia, almanusura imtoe uhai wake или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
RAIS John Magufuli amesema utendaji wake wa kazi ambao ulimfanya Rais Benjamin Mkapa akiwa madarakani wakati huo amsifie hadharani, ulisababisha anyweshwe sumu na ilibaki kidogo apoteze maisha. Ameyasema hayo Jumanne, Novemba 12, 2019, katika uzinduzi wa kitabu cha rais mstaafu Benjamin Mkapa kiitwacho cha ‘My Life, My Purpose’ (Maisha Yangu, Kusudio Langu) uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. “Nilipofanya kazi vizuri Mzee Mkapa hakusita kunisifia na sitosahau siku aliyotangaza kuwa mimi ni askari wake wa mwamvuli, baada ya kutangazwa hivyo nilichukiwa na viongozi wengine tena wa ngazi za juu hadi kufikia hatua ya kunyweshwa sumu Dodoma,” alisema. “Nashukuru Mungu baada ya kunyweshwa sumu na kupona, nilienda kwa Mzee Mkapa na kumueleza azma yangu ya kujiuzulu, nakumbuka aliniangalia kwa jicho la baba na mwana akanipa ujasiri na kuniambia usijiuzulu, akanipa ulinzi na nikaendelea kuchapa kazi. “Katika tukio hilo nilimuona Mzee Mkapa kama mtu anayekupa matumaini wakati wewe ukiwa umekata tamaa. Mzee Mkapa nakushukuru sana, nimejifunza kutowasifu wateule wangu hata kama wanafanya mazuri mengi, yasije yakawatokea yaliyonikuta mimi wakati uliponisifia,” amesisitiza Magufuli.