У нас вы можете посмотреть бесплатно WAZIRI MAVUNDE AZINDUA HELIKOPTA YA UTAFITI WA MADINI KAHAMA MAGANGILA ACHEKELEA FURSA ZA AJIRA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, leo amezindua helikopta ya kisasa ya utafiti wa kijiolojia wa anga inayomilikiwa na Kampuni ya Barrick, inayotekeleza shughuli zake kwa ubia na Serikali kupitia Twiga Minerals, kwa lengo la kuboresha utafutaji wa madini na kupunguza athari za kimazingira. Uzinduzi huo umefanyika Wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga, ambapo Waziri Mavunde amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuimarisha sekta ya madini nchini na kufungua fursa mpya za tafiti kwa kutumia teknolojia ya kisasa zaidi. Amesema uwekezaji katika teknolojia ya kisasa ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa Sera ya Madini ya Taifa inayolenga kuimarisha utafiti wa rasilimali madini, kuongeza mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa, pamoja na kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinafanyika kwa ufanisi na tija. Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa Barrick nchini, Dkt. Melkiory Ngido amesema uzinduzi wa helikopta hiyo ni hatua kubwa kwa kampuni hiyo katika kuendeleza ushirikiano wake na Serikali, kwani itasaidia shughuli za utafutaji wa madini kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ya utafiti wa kijiolojia wa anga. Dkt. Ngido ameongeza kuwa uzinduzi wa utafiti huo unaakisi dhamira ya Barrick kuendelea kuwekeza nchini na kubaini maeneo yenye uwezekano wa kuanzishwa migodi mikubwa itakayochangia maendeleo ya taifa kwa muda mrefu. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe.Mboni Mhita amesema Serikali ya Mkoa itaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji ili waweze kutekeleza shughuli zao kwa ufanisi, huku Serikali ikiendelea kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Naye Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. @magangilamabula , kwa niaba ya wananchi, amesema ujio wa helikopta hiyo ya utafiti wa madini unatarajiwa kuchochea uchumi wa wananchi mmoja mmoja kupitia migodi mipya itakayoweza kuanzishwa.