У нас вы можете посмотреть бесплатно Mavunde ametangaza nia kugombea jimbo la Mtumba, ataja sababu za kuihama Dodoma Mjini или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mbunge wa Dodoma Mjini (CCM), Anthony Mavunde ametangaza katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 atagombea tena ubunge katika Jimbo jipya la Mtumba, akianisha sababu tatu za kuiacha Dodoma Mjini. Uamuzi huo ameutangaza huku akilia kuwa hakuna namna na hawezi kujigawa katika maeneo mawili akabaki salama. Mavunde ambaye ni Waziri wa Madini ametangaza uamuzi huo leo Alhamisi Mei 15, 2025 mbele ya wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Ametaja sababu ya kuhama Jimbo la Dodoma Mjini ni ni amani ya nafsi, pia kuendeleza ujenzi wa barabara za Ihumwa, Hombolo hadi Mayamaya na Ntyuka -Mvumi ambao alianzisha. Pia mradi mkubwa wa Hombolo Thematic City na Bandari kavu ya Ihumwa. Mei 12, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Jaji Jacobs Mwambegele alitangaza mgawanyo mpya wa majimbo uliosababisha kuzaliwa kwa majimbo mapya manane ya uchaguzi na kufikisha jumla ya majimbo 272, Tanzania Bara na Zanzibar.