У нас вы можете посмотреть бесплатно Swahili: Jinsi ya Kujitayarisha kwa Uwezekano wa Kuzuiliwa au Kukamatwa na ICE или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
How to Prepare for Possible ICE Detention or Arrest Jinsi ya Kujitayarisha kwa Uwezekano wa Kuzuiliwa au Kukamatwa na ICE Hii ni video kuhusu mambo unayoweza kufanya ili kujitayarisha kwa uwezekano wa kuzuiliwa na ICE, na nini cha kufanya iwapo wewe au mpendwa wako atakamatwa au kuzuiliwa na ICE. Taarifa hii imeandaliwa mahsusi kwa watu wote wanaoishi Vermont na eneo la New England, lakini pia inawahusu watu kote nchini Marekani. Kuna taarifa nyingi katika video hii, na zote ni muhimu sana. Chukua muda wako kuitazama kwa makini, na ushiriki na familia pamoja na marafiki zako. Kabla hatujaanza, haya ni mambo matatu muhimu zaidi ya kukumbuka: Usi saini chochote unachopewa na mafisaa wa ICE inayo maanisha uhamiaji na forodha ya Merikani kabla hujazungumuza na wakili kuhusu hilo —Maafisa wa ICE wanaruhusiwa kukudanganya. Hifadhi kwa kukariri nambari ya simu ya mtu unayemwamini nchini Marekani, pamoja na A# yako (ikiwa unayo). Hi ni alien number nambari ya utambulisho wauhamiaji ya tarakimu Tisa Kusanya hati halisi au nakala za nyaraka ZOTE za uhamiaji na utambulisho wako, na uzihifadhi mahali salama ambapo mtu unayemwamini anaweza kuzipata kwa urahisi iwapo wewe au mpendwa wako mtazuiliwa. Huu ni muhtasari mfupi wa haki mbalimbali ambazo wahamiaji wanazo nchini Marekani. Taarifa hii pia inapatikana kwa urahisi mtandaoni. Angalia sehemu ya maoni ya video hii kwa viungo na maelezo zaidi. Napa nchini Marekani, “hadhi ya uhamiaji” kimsingi ni ruhusa ya kuwa na haki fulani. Kwa ujumla, Rais wa Marekani ndiye anayesimamia masuala ya uhamiaji. Hata hivyo, kuna SHERIA muhimu za uhamiaji nchini Marekani ambazo Rais hawezi kuzibadilisha. Lakini mahakama za uhamiaji zinaweza kubadilisha jinsi sheria hizo zinavyofafanuliwa na kutumika. Watu wenye aina tofauti za hadhi ya uhamiaji wana haki tofauti. Ikiwa huna hadhi ya uhamiaji: Una haki ya kukaa kimya iwapo afisa wa ICE atakuuliza maswali. Si lazima kila wakati uonyeshe kitambulisho kwa afisa wa ICE. Wahamiaji walioko kwenye mpaka wa Marekani wanaweza kuombwa waonyeshe uthibitisho wa hadhi yao ya uhamiaji, na unaweza kuchagua kutii au kutotii. Hata hivyo, kumbuka kwamba kukataa kuonyesha uthibitisho kunaweza kuwa sababu ya kuzuiliwa. Ikiwa umeomba hifadhi (asylum) au aina nyingine ya msaada au hadhi ya uhamiaji, basi ni lazima uonyeshe kitambulisho chako iwapo afisa wa uhamiaji atakiomba. Watu wote waliopo Marekani wana haki hizi za msingi: Huna wajibu wa kumruhusu afisa wa ICE au afisa wa polisi kuingia nyumbani kwako bila kibali cha mahakama kilicho na sahihi ya hakimu wa Marekani. Ikiwa afisa wa ICE watadai usaini nyaraka zozote, una haki ya kukataa kusaini hadi upokee na kuelewa nakala ya hati hiyo katika lugha yako ya asili. Una haki ya kukataa kusaini kitu chochote utakachopewa na afisa wa ICE. wanaruhusiwa kutumia njama za uongo kuhusu hati, hivyo huna wajibu wa kusikiliza wanachosema. Pia, waajiri kwa kawaida wanaweza kuweka utaratibu kwamba mtu mmoja tu (kama vile mwajiri) ndiye anayeruhusiwa kuzungumza na afisa wa ICE mahali pa kazi. Wafanyakazi wanapaswa kuwajulisha maafisa wa ICE kuhusu utaratibu huo na kwa heshima kukataa kuwaruhusu kuingia maeneo binafsi au kupata vifaa kama kompyuta bila kibali cha mahakama. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu haki zako kwa kuangalia sehemu ya maoni ya video hii. Serikali hairuhusiwi kukiuka haki ambazo mtu anazo kulingana na hadhi yake ya wakati huo. Lakini idara la ICE na sehemu nyingine za serikali hazifuati kila wakati taratibu zao wenyewe. HIVYO BASI ICE au serikali wanapokiuka haki zako, ni muhimu kujua cha kufanya. Haki Zinapokiukwa: Kwa Sasha hive, chini ya uongozi wa Rais wa Marekani, si swali la “KAMA” haki zako zitakiukwa, bali ni swali la “LINI” haki zako zitakiukwa na idara la ICE au sehemu nyingine za mfumo wa uhamiaji wa Marekani. Kwa sasa, njia kubwa ambayo serikali inakiuka haki za watu ni mahali ambapo ICE wanapokamata na kuzuilia watu kwa kutumia mbinu au sababu zisizo halali kisheria. Njia nyingi ya kukamatwa na kuzuiliwa huko kunaweza kupingwa na wewe au wakili wako, lakini inaweza kuwa vigumu kujua cha kufanya. Kits cha Cha Kufanya ikiwa Wewe au Mpendwa Wako Mkizuiliwa: Kwa bahati mbaya, Vermont haina wakili wa kutosha wa uhamiaji kuwawakilisha kila mtu anayezuiliwa na ICE huko Vermont. Tarajia video ijayo yenye maelezo zaidi kuhusu namna ya kupata au kufanya kazi na wakili huko Vermont. Kwa sasa, fahamu kwamba mawakili lazima wafuate kanuni fulani za kisheria zinazowaruhusu kushughulikia kesi fulani tu na kuomba mambo fulani kutoka kwa serikali ya Marekani inayosimamia uhamiaji. Na kanuni hizi zinaweza kubadilika kighafla. Vermont inatoa rasilimali kwa jamii ya wahamiaji pale mtu anapokamatwa au kuzuiliwa na idara la ICE huko Vermont: Unaweza kuripoti kukamatwa na ICE kupitia Simu ya Dharura ya Migrant Justice: (802) 881-7229. Nambari hii ni kwa ajili ya taarifa za kukamatwa na kuzuiliwa pekee. Unaweza KUJAZA FOMU YA KUOMBA MSAADA WA KISHERIA kupitia VAAP.org/help (Cont...)