У нас вы можете посмотреть бесплатно WANANCHI KISA, MILEPA NA KINAMBO WAISHUKURU SERIKALI KWA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
WANANCHI KISA, MILEPA NA KINAMBO WAISHUKURU SERIKALI KWA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA Wananchi wa vijiji vya Kisa, Milepa na Kinambo wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuboresha miundombinu ya barabara katika vijiji hivyo, hatua inayolenga kurahisisha usafiri na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Wakizungumza na Wasafi Media, wananchi hao wamesema awali shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi zilikuwa zikikwama kutokana na changamoto ya usafiri, hasa wakati wa mvua, ambapo wamiliki wa vyombo vya moto walishindwa kuvuka kutoka upande mmoja kwenda mwingine. Wananchi hao wameeleza kuwa hali hiyo ilisababisha athari kubwa kwa jamii, ikiwemo baadhi ya wanafunzi kukatisha masomo, wanawake wajawazito kujifungulia njiani, huku wengine wakipoteza maisha kutokana na kushindwa kupata huduma za afya kwa wakati. Kwa upande wake, Mhandisi Mgeni Mwanga, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) amesema ujenzi wa madaraja hayo umegharimu jumla ya shilingi milioni 23.1 na umekamilika kwa asilimia 100, ambapo utekelezaji wake umefanywa na mkandarasi Stecol Corporation kutoka China. Aidha, Mhandisi Mgeni amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira kwa kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu katika mito na pembezoni mwa barabara, ili kuzuia mmomonyoko wa udongo na kulinda miundombinu hiyo kwa matumizi ya muda mrefu. SUBSCRIBE channel hii kupata habari kubwa zinazobamba mtandaoni / @kakwaletv Like us on Facebook, / kakwaletvtz Follow us on Twitter, / kakwaletv Follow us on Instagram, / kakwaletv