У нас вы можете посмотреть бесплатно DKT. DANIEL MONO ACHAGULIWA KUMRITHI ASKOFU SENDORO DAYOSISI YA MWANGA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mchungaji Dkt. Daniel Mono, Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (DKMZV), amechaguliwa kuwa Mkuu Mteule wa Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Uchaguzi huo ulifanyika leo katika mkutano mkuu maalumu uliofanyika katika kanisa kuu Mwanga ya Dayosisi hiyo. Dkt. Alex Malasusa, Mkuu wa KKKT na msimamizi wa uchaguzi, alisema kuwa Dayosisi ya Mwanga imeonyesha ukomavu na mkutano huo ulikuwa wa amani na upendo. Viongozi mbalimbali wakiwemo Askofu Syprian Yohana Hilint wa Dayosisi ya Kati Singida na Mbunge wa Jimbo la Mwanga, Joseph Tadayo, walieleza matarajio yao kwa Askofu aliyechaguliwa kuwa kazi ya Mungu itaendelea kwa ufanisi. Katika uchaguzi huo, Dkt. Mono alipata kura 127 za ndiyo, sawa na asilimia 96.2, kati ya kura 132 zilizopigwa. Kura za hapana zilikuwa tano.