У нас вы можете посмотреть бесплатно MKUU WA MKOA WA IRINGA KATIKA MAHAFALI YA 4 YA CHUO CHA TURNBULL TECH COLLEGE -MGENI RASMI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
RC KHERI JAMES AWASHA MOTO WA MAENDELEO KWA VIJANA Mkuu wa Mkoa wa Iringa, pia Mhe.Kheri James, amezielekeza Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa, kuhakikisha zinatenga maeneo maalum kwa ajili ya vijana wanaomaliza masomo yao katika vyuo vikuu na vya kati, kwa lengo la kuwawezesha vijana hao kutumia maeneo hayo kwaajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi, ili kuchangia maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla. Ameyasema hayo leo Julai 26,2025 katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo,wakati wa Mahafali ya Nne ya Chuo cha Turnbull Tech Training College kilichopo Kihesa Majembe,Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, ambapo Mhe. Kheri amesema kuwa hatua hiyo inalenga kuwasaidia vijana kuwa wabunifu, kuanzisha miradi mbalimbali ya uzalishaji mali na kuondokana na utegemezi baada ya kuhitimu masomo yao. “Tuna vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu kila mwaka, lakini changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ukosefu wa rasilimali na maeneo ya kuanzia shughuli za kiuchumi. Ni wajibu wa halmashauri zetu kutambua kundi hili na kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha kujiajiri na kuchangia pato la Taifa,” Mhe. Kheri Ameongeza kwa kusema kuwa Serikali ya Mkoa ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha vijana wanapata msaada wanaohitaji ili kufanikisha malengo yao ya kiuchumi huku akisisitiza kuwa maeneo yatakayotengwa yanaweza kuwa ya kilimo, biashara ndogondogo, viwanda vidogo kulingana na mahitaji na uwezo wa vijana hao. Akitoa Taarifa,Mkurugenzi wa Chuo hicho Ndg. Daudi Kingalata amesema kuwa Changamoto kubwa inayowakabili ni kukosa eneo la kujenga Chuo hicho ikiwa kwa sasa wamepanga katika maeneo ambayo shughuli nyingi za kijamii zimekuwa zikifanyika, ambapo Mhe. Kheri ameutaka uongozi huo kuandika barua za kuomba eneo la kujenga chuo katika Halmashauri zote zilizopo mkoani hapa. Nao Baadhi ya Wahitimu wa Chuo hiki wametoa shukrani kwa serikali ya mkoa huku wakiahidi kwenda kuyafanyia kazi yale yote waliyojifunza. #iringaimaratutaijengakwaumojanauwajibikaji / dmlzer. .