У нас вы можете посмотреть бесплатно WAZIRI SILAA AIPONGEZA IAA KWA KUTOA MAFUNZO KWA VITENDO KUPITIA KIATAMIZI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Vituo Atamizi (Incubation Hubs) ikiwemo IAA Business Starup Centre (IBSUC) vimekuwa na umuhimu mkubwa katika kujenga, kulea na kutengeneza mawazo na bunifu za vijana wenye kampuni changa, ili kuhakikisha wanafikia malengo na kuleta suluhu za changamoto mbalimbali katika jamii Hayo yameelezwa leo Machi 12, 2025 na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry Silaa (MB) katika Ziara ya kikazi katika Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA), alipotembelea na kuzungumza na Jumuiya ya wanafunzi na wahadhiri kuhusiana na masuala ya Kampuni changa za wanafunzi hususani zilizojikita katika matumizi ya TEHAMA Waziri Silaa ameupongeza uongozi wa IAA kwa kazi nzuri ya kuandaa mazingira wezeshi ya kulea na kukuza mawazo ya vijana pamoja na bunifu zao kupitia kiatamizi cha (IBSUC), ili kuweza kutoa wahitimu wenye uwezo wa kutumia taaluma zao katika kuleta suluhu ya masuala mbalimbali Pamoja na kuweza kujiajiri baada ya masomo Aidha, Waziri Silaa amesema wizara itahakikisha inashirikiana na Chuo katika kuhakikisha wanawashika mkono wanafunzi katika bunifu zao ili kuweza kuwasaidia kufikia malengo waliojiwekea Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Utafiti na Ushauri IAA Dr. Grace Idinga amesema IAA inajivunia kuwa na vijana wabunifu ambao wamekuwa wakishiriki katika mashindano mbalimbali ya TEHAMA, na kufanya vizuri, na pia uongozi wa Chuo una mkakati wa kujenga kituo cha TEHAMA ili kutoa mafunzo ya teknolojia kwa wanafunzi. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Kitivo cha Tehama, Mohamed Mwanga amemshukuru Waziri Silaa kwa Ziara yake IAA na kusema kuwa Kitivo cha TEHAMA kitaendelea kuwezesha bunifu za wanafunzi na kuiomba Wizara isichoke kutoa kuwashika mkono kwa manufaa ya Chuo na Taifa kwa ujumla