У нас вы можете посмотреть бесплатно 🔴 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema hadi kufikia saa 10 jioni leo Desemba 3, 2023 watu 47 wamefariki dunia na wengine 85 kujeruhiwa wilayani Hanang kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo. Mvua hiyo ilisababisha sehemu ya Mlima Hanang kumomonyoka na kusababisha kutiriika kwa tope katika maeneo ya Katesh na Gendabi. Sendiga amesema watu wengine wanahofiwa kufukiwa na tope baada nyumba na makazi yao kusombwa na mafuriko na maporomoko ya udongo huo kutoka Mlima Hanang. Akizungumza na waandishi wa habari amesema eneo kubwa lililoathiriwa na mafuriko hayo ni Kata ya Gendabi na katikati ya Mji wa Katesh ambayo ni makao makuu ya Wilaya ya Hanang mkoani Manyara. "Nyumba za watu zimezingirwa na mafuriko na miti iliyosombwa na mafuriko kutoka sehemu ya mlima Hanang yamesababisha barabara ya Katesh kwenda Singida kushindwa kupitika," amesema Sendiga.