У нас вы можете посмотреть бесплатно JAFO AUNDA KAMATI KUCHUNGUZA WAGENI WANAOFANYA BIASHARA YA 'UMACHINGA' NCHINI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Jafo aunda kamati kuchunguza wageni wanaofanya biashara ya ‘umachinga’ nchini Siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutaka uchunguzi juu ya wageni wanaofanya biashara zinazofanywa na wazawa, Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo, ameunda kamati ya watu 15 kuchunguza changamoto hiyo. Kumekuwa na malalamiko ya ongezeko la raia wa kigeni wanaofanya biashara za rejareja (machinga), hali inayowaathiri wafanyabiashara wazawa katika soko la Kariakoo. Waziri Jafo ametangaza hatua hiyo leo Jumapili Februari 2, 2025 jijini Dar es Salaam, huku akibainisha kuwa kamati hiyo itakayoongozwa na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Edda Lwoga, itafanya kazi kwa muda wa siku 30 na itaanza kazi hivi karibuni. Amesema lengo la kamati hiyo ni kufanya uchunguzi wa kina kuhusu biashara za wageni nchini, kuchambua vibali na leseni wanazopatiwa na kubaini maeneo yenye changamoto kubwa. Video na Ally Mlanzi