У нас вы можете посмотреть бесплатно Dayna Afunguka Siri Mpaka Kupata Collabo Na Davido "Sikuwa Nimefurahi" | SALAMA NA DAYNA NYANGE PT 2 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 Dayna Nyange ni shujaa, mpambanaji, Mama, Dada na mengine mengi ila kubwa zaidi ambalo mimi na wewe limetufanya tumfahamu ni MWANAMUZIKI, tena HODARI haswa. Na ambacho mimi kinanivutia zaidi ni jinsi ambavyo amekua akipambania ndoto yake kwa muda mrefu, hivi karibuni karata zake ambazo amekua akizicheza kwa muda mrefu zimeanza kutoa makopa na almasi ambazo zilitakiwa zije muda mrefu tu. Yeye kakuzwa na Marehemu Bibi yake (Mwenyezi Mungu Amrehemu) ambaye kwa mujibu wa Dayna alikua ni rafiki yake. Alimfunza mambo mengi na alikua mkweli mbele yake. Alikua mkarimu pia na kipenzi cha kweli cha Dayna. Alizaliwa na kupewa jina la Mwanaisha Said Nyange, jina ambalo si wengi wanaofahamu nalo. Pengine aliona ki muziki lisingeleta amsha amsha ambayo Dayna limeleta. La kipekee na linashikika. Au pengine sababu za kidini nazo zilipelekea yeye kufanya hivyo. Sikutaka tuyaongee haya ya jina kwa kina, sikutaka kumfanya awe uncomfortable maana mengi ambayo tumeyaongea yalikua tayari yamemfanya asiwe kwenye eneo lake la kujidai na kuwa huru. Kuongelea yalopita si kila mmoja anakua tayari pengine kwasababu mengi ya nyuma hatuyapendi au hatujivunii nayo au utayari wa kuyazungumzia hatuko nao. Kwa heshima tulonayo kati yetu nadhani ndo ili fanya iwe rahisi kwa sisi kuongea, tulianzia nyuma kutoka siku ya kwanza ambayo mimi na yeye tulikutana mara ya kwanza, ilikua studio moja hivi mjini Morogoro, na Dayna ananikumbusha kwamba tayari pale alikua na mtoto wake. Na alikua kashaolewa, mume alikua anaenda kazini na yeye alikua anafanya mambo yake mengine, ya muziki hayo ambayo ndo aliyokua anayapenda na mpaka leo anayapenda na kuyafanya. Simulizi za yeye kuolewa akiwa na umri mdogo, za kuachana na aliyekua mpenzi wake na kuolewa na mtu mwengine, kutoroka nyumbani na kwenda kukutana na huyo mtu mwengine wakiamini pengine bado inawezekana wao kuwa pamoja. Mahusiano yake na Bibi yake, na Baba yake na Mama yake ambaye alimjua baadae sana. Siku zote wakati anakua, Dayna alijua Bibi yake ndiye Mama yake. Upendo ambao alikua anamuonyesha ulikua ni kabisa kama wa Mama na mtoto wake. Sababu za ndoa kuvunjika, jinsi alivyong’amua kuhusu Mama yake, kuhusu Baba yake. Safari yake ya muziki mpaka leo hii. Mahusiano yake na binti yake ambaye Dayna anatuambia ni hodari sana shuleni, mahusiano yake na Baba wa mtoto wake. Maisha ya sasa na jinsi ambavyo amepambana na anavyoendelea kupambana ili azidi kuwepo, ni baadhi ya mambo tuliyoyaongelea humu. Yangu matumaini, utamuangalia kwa heshima zaidi na kumtakia KHERI zaidi maana alipotoka si karibu na anapoenda kwa Rehema za Mwenyezi Mungu atafanikisha tu ndoto zake. Tafadhali enjoy, Love, Salama. Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One The Incredible & Msam... Follow: Twitter: / yahstonetown Instagram: / yahstonetown Facebook: / yahstonetown Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz