У нас вы можете посмотреть бесплатно Fahamu Kazi na Majukumu ya TCRA kwa Mujibu wa Sheria или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
UTANGULIZI Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ni Taasisi ya Serikali yenye jukumu la kusimamia Sekta ya Mawasiliano nchini Tanzania. Sekta ya Mawasiliano inajumuisha Utangazaji, Simu na Intaneti, na Posta. TCRA ilianzishwa chini ya Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Namba 12 ya mwaka 2003 baada ya kuunganishwa kwa iliyokuwa Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC) na Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC). TCRA ilianza kutekeleza majukumu yake tarehe 1 Novemba 2003. Kazi na Majukumu ya TCRA kwa Mujibu wa Sheria Kwa mujibu wa Kifungu Na. 5 cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya 2003, TCRA ina wajibu wa: - 1. Kuhimiza ushindani bora na uchumi wenye tija; 2. Kulinda haki na maslahi ya watumiaji; 3. Kuhamasisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa watumiaji wote ukijumuisha watumiaji wenye kipato kidogo, walioko vijijini na watumiaji ambao wako katika maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara; 4. Kuimarisha elimu kwa umma, uelewa na kuzifahamu huduma zinazosimamiwa na TCRA; na Kuhakikisha umuhimu wa kulinda na kutunza mazingira. Fahamu zaidi: bit.ly/KuhusuTCRA