У нас вы можете посмотреть бесплатно KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 12/02/2026 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 12/02/2026 UJUMBE WA LEO: MAMBO YATAKAYOKUWEZESHA KUTOKA NYUMBA YA UTUMWA MPAKA UTIMILIFU WA AHADI Kutoka 20 : 1 - 2 Mwanzo 49 : 22 - 26 Mwanzo 50 : 24 - 26 1. Kuelewa Safari ya Ukombozi na namna udhihirisho wa mkono wa MUNGU kuingilia kati hali za watu wake waliopo kwenye nyumba ya utumwa. 2. Nafasi ya Agano la urithi na mauti kutoka kwenye madhara yake ili kunufaika kwa kutoka katika nyumba ya Utumwa. 3. Kujua dalili ya vita inayolenga kipawa chako, ili kubakia utumwani kama lengo la Adui kisitumike kukutoa Utumwani. Kutoka 20 : 1 - 2 1 Mungu akanena maneno haya yote akasema, 2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Mwanzo 49 : 22 - 26 22 Yusufu ni mti mchanga wenye kuzaa, Mti mchanga wenye kuzaa karibu na chemchemi, Matwi yake yametanda ukutani. 23 Wapiga mishale walimtenda machungu, Wakamtupia, wakamwudhi, 24 Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli, 25 Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba. 26 Mibaraka ya baba yako Imepita mibaraka ya milima ya kale, Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele; Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu, Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake. Mwanzo 50 : 24 - 26 24 Yusufu akawaambia nduguze, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo. 25 Yusufu akawaapisha wana wa Israeli, akasema, Bila shaka Mungu atawajia ninyi, nanyi mtaipandisha huko mifupa yangu. 26 Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia na kumi; wakampaka dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri. Waebrania 9 : 16 - 17 16 Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. 17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya. SAFARI YA UKOMBOZI INA HATUA TATU. 1. Mungu anaona utumwa. 2. Mungu anaingilia kwa mkono wake 3. Mungu anatimiza ahadi yake kwa wakati wake. MIFUPA YA YUSUFU ▶️ Imani isiyokufa ▶️ Tumaini la ahadi za Mungu ▶️ Uaminifu wa Mungu katika agano ▶️ Urithi na maono ya vizazi ➡️ Kifo cha Yusufu kilifungua msimu mpya wa kuzaa taifa. Kwa lugha ya agano: ▶️ Mbegu ya Ibrahimu sasa iligeuka kuwa watu wengi. ▶️ Familia iligeuka kuwa taifa. BARAKA YA MUNGU KATIKA URITHI WA AGANO LA YUSUFU ▶️ Kuwa karibu na Mungu ( chemchemi ) huleta matunda. ▶️ Upinzani hauzuii kusudi la Mungu. ▶️ Mungu ni mwamba, mchungaji, na mwenye nguvu katika nyakati zote. ▶️ Baraka za Mungu ni kamili kiroho, kimwili, na kizazi. ▶️ Uaminifu katika majaribu huleta kuinuliwa. Mhubiri : Mwl.Renald Mlawi. Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com