У нас вы можете посмотреть бесплатно Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Yatoa Elimu ya Sheria ya Ustawi wa Wanyama kwa Wafugaji Dodoma или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Yatoa Elimu Kuhusu Sheria ya Ustawi wa Wanyama kwa Wafugaji Katika Maonesho ya Nanenane Dodoma Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) imeendelea kutoa elimu ya sheria kwa wananchi wanaoshiriki katika Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma ambapo elimu juu ya Sheria ya Ustawi wa Wanyama, Sura Na. 154, ilitolewa kwa makundi mbalimbali ya wafugaji kutoka mikoa tofauti ya Tanzania. Akizungumza mara baada ya kukutana na wafugaji hao wakili wa serikali kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Vick Mbunde amesema kuwa lengo kuu la elimu hiyo ni kuwawezesha wafugaji kufahamu haki za wanyama wanaowafuga na wajibu wao katika kuwahudumia wanyama hao, kama sheria inavyoainisha. “Wafugaji wengi hawafahamu uwepo wa sheria inayowataka kuwahudumia vyema wanyama wao, ikiwemo kuhakikisha wanapata chakula cha kutosha, maji safi, malazi bora, na matibabu. Sheria ya Ustawi wa Wanyama inalinda maslahi ya wanyama dhidi ya mateso, manyanyaso na mazingira duni ya maisha,” alisema Vick. “Sheria ya Ustawi wa Wanyama, Sura Na. 154, inalenga kuhakikisha kuwa wanyama wote wanaofugwa au kutunzwa na binadamu wanapokea huduma stahiki, na inatoa adhabu kwa yeyote anayekiuka masharti ya sheria hiyo”. Alisema Katika maonesho hayo, Tume pia imekuwa ikigawa vipeperushi vyenye maelezo ya msingi kuhusu Sheria hiyo pamoja na kutoa nafasi kwa wananchi kuuliza maswali na kupata majibu ya kitaalamu kuhusu masuala ya kisheria yanayohusu mifugo na wanyama kwa ujumla. Hosea Godwin Mfugaji anasema ameipongeza Tume hiyo kwa jitihada hizo kwamba elimu iliyotolewa imewasaidia kufahamu masuala ambayo hapo awali hawakuyatilia maanani. “Nilikuwa sifahamu kuwa ukimtesa mnyama, kama kumpiga hovyo au kumwacha bila chakula kwa siku kadhaa, ni kosa na unaweza kuchukuliwa hatua za kisheria. Hii ni elimu muhimu sana kwetu sisi wafugaji,” alisema Tume ya Kurekebisha Sheria inatarajia kuendelea na kampeni zake za kutoa elimu ya sheria katika maeneo mbalimbali nchini, kwa lengo la kujenga jamii inayozingatia sheria na haki za kila kiumbe hai.