У нас вы можете посмотреть бесплатно MUUAJI WA VIKONGWE, WAZEE ANASWA TABORA, "alikua anatishia uhai wetu" или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Tabora vimefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa wa mauaji ya vikongwe katika mkoa huo ambaye alikuwa akitafutwa kwa zaidi ya miaka 10 bila mafanikio ambapo amekamatwa wilayani Uyui mkoani humo. Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo, amesema wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya vikongwe katika mkoa huo ambaye alikuwa akitafutwa tangu mwaka 2013. Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Oktoba 2, Paul Chacha amesema mtuhumiwa huyo amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu na hatimaye amekamatwa wilayani Uyui akijiandaa kutoroka baada ya wasamalia wema kutoa taarifa za uwepo wake. “Yupo mtuhumiwa wa ujambazi ambaye alikuwa anakodiwa kuwaua vikongwe tangu mwaka 2013 vyombo vya ulinzi vimekuwa vikimtafuta bila mafanikio na kipindi hicho mauaji ya vikongwe hapa Tabora yalikithiri lakini ninavyosema leo tumeshamkamata na yuko kwenye mikono ya serikali akingojea sheria ichukue mkondo wake,“ alisema na kuongeza “tulimkatama wilayani Uyui kijiji cha Kizenga, kinachofuata kwa sasa ni taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea ili aweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili aweze kujibu tuhuma zinazo mkabili katika kipindi chote ambacho alikuwa akijihusisha na mauaji kwa muda mrefu” alisema chacha Hata hivyo RC Chacha amesema watu wengine watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kuozesha watoto wadogo katika mkoa huo. “watoto watatu wa familia moja waliozeshwa ambapo mtoto wa kwanza alilipiwa mahali ya ng’ombe 48 na mwingine akalipiwa ng’ombe 22 sasa waoaji na hawa wazazi tumewakamata na tumewafikisha kwenye vyombo vya sheria “ alisema Katika hatua nyingine chacha amesema Serikali ya mkoa huo inafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha Amani inaendelea kuwepo katika mkoa huo jambo litakalowafanya wananchi wake wafanye kazi kwa uhuru muda wote. Alipotafutwa Raphael Kinoji mkazi wa Mshikamano Tabora amesema kukamatwa kwa wahalifu hao kutasaidia watu kupumua. “naipongeza vyombo vya usalama kwa kumkamata huyu muuaji wa vikongwe, sisi wazee tulikuwa hatuishi kwa Amani maana alikua anatishia uhai wetu kwakweli lakini sasa tutapumua kwakua ameshakamatwa” Kwa upande wake Esta Philemon mkazi wa manispaa ya Tabora anasema serikali inatakiwa iendelee kuwasaka wahalifu kwakua kumkatama mtu mmoja hainamishi kwamba tatizo litapungua. “nalipongeza jeshi la polisi na Mkuu wa mkoa kwa kumkamata huyo mtuhumiwa wa mauaji lakini nashauri kwamba wahalifu wengine waendelee kutafutwa kwakuwa mpaka kufikia hatua ya kuua hawezi kuwa peke yake, hivyo doria ziendelee ili wakamatwe wengine zaidi” amesema. Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao kutaka kujua zaidi kuhusiana na kukamatwa mtuhumiwa huyo, amesema bado kuna uchunguzi unafanyika na ukikamilika taarifa zitatolewa.