У нас вы можете посмотреть бесплатно VIJANA WAPATIWA MITAJI KUTOKANA NA AHADI YA WAZIRI JOEL NANAUKA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
VIJANA WAPATIWA MITAJI KUTOKANA NA AHADI YA WAZIRI JOEL NANAUKA Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mhe. Aida Clarence Haule, amekabidhi kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kama mitaji kwa vijana wawili wa Mbalizi waliowasilisha ombi lao kwa Waziri wa Vijana, Mhe. Joel Nanauka, wakati wa ziara yake hivi karibuni. Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Aida amewapongeza vijana hao kwa kuonyesha uthubutu na moyo wa kujiendeleza kupitia biashara zao ndogo. Amesisitiza kuwa ofisi za Halmashauri zipo wazi kwa ajili ya kuwahudumia vijana wote na kuwaelekeza kwenye fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali. Aidha, Mhe. Aida amewahimiza vijana wengi zaidi kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani, ili kukuza biashara zao na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla. Kwa upande wake, Katibu wa Wamachinga, Bw. Clemence Mwaitebele, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha Wizara ya Maendeleo ya Vijana, akisema imekuwa jibu la muda mrefu kwa changamoto za vijana. Pia amepongeza Halmashauri kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi ya Mhe. Waziri. Vijana hao walimuomba Waziri Nanauka kuwaongezea mitaji walipokutana naye katika stendi ya mabasi Mbalizi, na ahadi hiyo sasa imetekelezwa rasmi.