У нас вы можете посмотреть бесплатно WAKAZI HIMO WALAANI TABIA KUWAFUNGIA WATOTO NDANI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Baadhi ya wakazi wa Himo, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamelaani tabia ya baadhi ya wazazi kuwafungia watoto ndani, wakisema ni hatari inayoweza kusababisha maafa. Wamesema hayo leo Jumanne Desemba 17,2024 wakati wa mazishi ya watoto wawili wa familia moja katika Kitongoji cha Darajani, waliofariki dunia kwa kuungua moto walipokuwa wakichezea jiko la gesi ndani ya nyumba yao. Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilitokea Ijumaa, Desemba 13, 2024, wakati mama wa watoto hao alipokuwa amewafungia ndani na kwenda kwenye shughuli zake za utafutaji. Jirani wa familia hiyo, Jane Mosha, amesema tukio hilo linapaswa kuwa somo kwa wazazi wote wenye tabia kama hiyo. “Tunalaani vikali tabia ya kuwafungia watoto ndani. Wazazi tunapokuwa na ugomvi na majirani tusihusishe watoto, kwa sababu watoto hawana makosa. Wazazi tujifunze kutoka tukio hili,” amesema. Awali Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi, alisema uchunguzi zaidi unafanyika kuhusu tukio hilo na taarifa kamili itatolewa baadaye. Watoto hao, Meshack Nyembo (3) na Pendo Nyembo (1), walifariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Faraja iliyopo Himo baada ya kuungua moto wamezikwa katika makaburi ya Mieresini Himo. Mazishi yao yameacha simanzi kubwa huku wakazi wa Himo wakihimizwa kujifunza kutokana na tukio hilo ili kulinda usalama wa watoto. (Imeandaliwa na Yese Tunuka na Ombeni Daniel )