У нас вы можете посмотреть бесплатно MTWARA; MWANAFUNZI APIGWA HADI KUFA NA MWALIMU WAKE или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwanafunzi wa kidato cha Tatu katika shule ya secondari ya Sabasaba iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara Mwanaid Ally mwenye umri wa miaka Kumi na Sita anadaiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na mwalimu wake baada ya kushindwa kujibu swali la darasani . Taarifa zinadai kuwa mwanafunzi huyo baada ya kupigwa alidondoka na kupoteza fahamu akiwa shuleni hapo ambapo mwanafunzi huyo anadaiwa kufanyiwa kitendo hicho Oktoba 20 mwaka huu. Mama mzazi wa mtoto huyo Amina Hamis amesema kuwa alipigiwa simu kutoka shuleni wakati akiwa kwenye shughuli zake na kuelezwa kwenda shuleni hapo kwa ajili ya kumfuata mtoto wake aliyedaiwa kupoteza fahamu bila kuelezwa sababu. Amesema alipofika shuleni alimchukua mtoto wake na kurudi naye nyumbani na kisha kufanya jitihada za kumsaidia hadi pale alipopata fahamu na kisha mtoto kuelezea kisa hicho kwa mama yake ambapo baadaye mama alienda kuripoti taarifa hizo polisi. Kufuatia tukio hilo Jeshi la polisi mkoani Mtwara limetoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kifo cha mwanafunzi huyo kwamba taarifa za kitabibu kutoka kwa daktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara ya Ligula inasema kifo cha mwanafunzi huyo kimesababishwa na kuvuja damu nyingi isiyoganda ambayo ilikuwa inatoka kwenye fizi za mdoni na kupelekea kupoteza damu nyingi .