У нас вы можете посмотреть бесплатно MWANAMKE ALIYEISHI NA MAITI YA MCHUNGAJI WAKE AKIAMINI ATAFUFUKA MBARONI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwanamke mmoja ajulikanaye kwa Jina la Agnes Mwakijale Mkazi wa Kitongoji cha Isakalilo (C) kata ya Kalenga, Wilaya ya Iringa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kukutwa akiishi nyumba moja na Mwili wa Marehemu ambaye alikuwa ni Mchungaji wake aliyetambulika kwa Jina la John Chida kwa muda wa miezi miwili akiwa na imani kuwa atafufuka. Katika hali isiyo ya kawaida Mwanamke huyo ambaye alikuwa ni muumini wake katika Kanisa la El-Huruma aliishi na Mwili huo wa Marehemu nyumba moja kwa takribani miezi miwili akivumilia harufu kali ya mwili huo huku akiamini ipo siku Mungu atamfufua kama ambavyo majirani wanaeleza. Hata Hivyo Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Isakalilo (C) Amosi Msole ameeleza namna ambavyo Mchungaji huyo alivyokuwa akikaidi kupelekwa Hospitali akiamini kuwa Mungu atamponya. Mwenyekiti huyo anaendelea kueleza siku ya tukio hali ilivyokuwa nyumbani hapo kwa Marehemu John Chida. Tayari mwili umeshachukuliwa na Jeshi la Polisi na Mtuhumiwa ameshikiliwa kwa Uchunguzi zaidi.