У нас вы можете посмотреть бесплатно TCAA YAANDAA IFTAR MAALUM KWA WATOTO WENYE UHITAJI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imeandaa futari maalum kwa watoto wenye uhitaji kutoka Kituo cha Kulea Watoto wenye Uhitaji cha Zili, tukio lililolenga kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuendeleza ujumuishi kwa makundi yenye mahitaji maalum. Hafla hiyo ilifanyika katika Makao Makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na wadau wa sekta ya usafiri wa anga, watumishi wa TCAA pamoja na watoto wenye uhitaji. Wageni walishiriki futari kwa pamoja na watoto hao, pamoja na kukabidhi zawadi kama ishara ya upendo, mshikamano na uwajibikaji wa kijamii. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile, aliyemwakilisha Waziri wa Uchukuzi, alipongeza jitihada za TCAA katika kuchangia maendeleo ya jamii akisisitiza umuhimu wa taasisi za umma kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii, hususan zinazolenga kuwajali watoto wenye uhitaji. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Salim Msangi alisisitiza kuwa pamoja na jukumu la kusimamia na kudhibiti sekta ya usafiri wa anga, mamlaka itaendelea kutekeleza miradi ya kijamii inayolenga kugusa maisha ya wananchi na kukuza maadili ya utu, mshikamano na usawa. Kupitia futari hii maalum, TCAA imeendelea kudhihirisha kuwa sekta ya usafiri wa anga siyo tu kuhusu usimamizi na kanuni, bali pia ni chombo muhimu cha kujenga jamii jumuishi, yenye huruma na mshikamano. Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ni taasisi ya umma yenye jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka iliundwa kwa Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 (R.E 2006). Majukumu ya kisheria ya Mamlaka ni kudhibiti masuala ya ki-usalama, ki-uchumi katika usafiri wa anga na kutoa huduma za uongozaji ndege. Pia Mamlaka inatoa huduma za uongozaji ndege kwenye vituo vya ndege kumi na nne (14) ambavyo ni: Dar es Salaam, Kilimanjaro,Tanga, Arusha, Mwanza,Tabora,Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Songea, Mtwara, Zanzibar na Pemba