У нас вы можете посмотреть бесплатно “Wajasiriamali Wanawake Singida Watakiwa Kuacha Uoga, Waelekezwa Njia za Kufanikiwa Kibiashara” или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wajasiriamali wanawake wa Wilaya ya Singida wametakiwa kujitofautisha na kuwa wabunifu katika biashara wanazozifanya ili kuongeza ushindani na kufikia mafanikio makubwa kiuchumi. Wito huo umetolewa jana Machi 3, 2026 wakati wa Kongamano la Wanawake Wilaya ya Singida, lililofanyika katika Manispaa ya Singida kuelekea Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani. Akitoa mada kuhusu uwekezaji na fursa za kiuchumi kwa wanawake, Mkuu wa Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Bi. Happiness Rugeimukamu, alisema wanawake wanapaswa kujenga kujiamini wanapoendesha biashara zao badala ya kuwa na hofu. Alisema kujiamini ni moja ya silaha muhimu kwa mfanyabiashara, hasa katika kipindi hiki ambacho ushindani wa kibiashara unaongezeka siku hadi siku. “Wajasiriamali wanatakiwa kujitofautisha wanapofanya biashara zao na kuwa wabunifu katika biashara wanazozifanya. Pia ni muhimu kufanya biashara kwa kujiamini ili kuweza kufanikiwa na kufika mbali,” alisema. Bi. Rugeimukamu alieleza kuwa wanawake wana uwezo mkubwa wa kufanya biashara na kuwekeza endapo wataamua kutumia vizuri fursa zilizopo pamoja na kuongeza ubunifu katika huduma au bidhaa wanazozalisha.