У нас вы можете посмотреть бесплатно ARURA yafuta ‘stendi bubu’ Arusha kupunguza foleni katikati ya jiji или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla ameiagiza TARURA, Jeshi la Polisi na TANROADS kushughulikia kwa haraka changamoto ya foleni ndani ya Jiji la Arusha ili kuondoa vikwazo kwa shughuli za kiuchumi na kijamii. Kufuatia agizo hilo, kikao kilichofanyika kimehusisha TARURA, LATRA, TANROADS, Polisi na Idara ya Mipango Miji, ambapo kimeamua kufuta vituo vya mabasi visivyo rasmi (stendi bubu) katikati ya jiji vinavyotumika kupakia na kushusha abiria, huku mabasi yote yakielekezwa kutumia Kituo Kikuu cha Mabasi Arusha. Akizungumza kwa niaba ya kikao hicho, Kaimu Meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha, Mhandisi Julius Kaaya amesema utekelezaji unaanza mara moja na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya kampuni zitakazokaidi agizo hilo. Naye Afisa Mipango Miji Jiji la Arusha, Bi. Doroth Absalom, amesisitiza kuwa ni kinyume cha sheria kutumia majengo ya makazi au biashara kama vituo vya mabasi, akionya pia dhidi ya uoshaji holela wa mabasi pembezoni mwa barabara, akieleza kuwa mabasi yote yanapaswa kuanzia safari zao katika Kituo Kikuu cha Mabasi Arusha. #arusha #tanzania #music #chuga