У нас вы можете посмотреть бесплатно MHE GILBERT TARIMO AKABIDHIWA KIJITI KUONGOZA ALAT MKOA KILIMANJARO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwenyekiti wa Kikao cha Uchaguzi cha ALAT mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. John Meela maarufu kama “Chui”, amemtangaza rasmi Mhe. Gilbert Tarimo ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mkoa wa Kilimanjaro kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2026 hadi 2030. Mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uchaguzi lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kwa kufuata taratibu na kanuni za ALAT, likiwahusisha wajumbe kutoka mamlaka mbalimbali za serikali za mitaa. Akitangaza matokeo hayo, Mhe. Meela alimtangaza Mhe. Gilbert Tarimo kwa kupata kura 14 huku msindani wake Mhe Edmund Rutaraka kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Hai akipata kura 13 na kura moja iliharibika ambapo jumla ya kura zote zilikuwa 28. Aidha katika uchaguzi huo wajumbe wamemchangua Yusto Mapande Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same kuwa Makamu Mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Kilimanjaro akiwa mgombea pekee aliyepigiwa kura za ndio na hapana kwa kupata kura 27 na moja ikiharibika. Mhe Meela amempongeza Gilbert Tarimo kwa kuaminiwa na wajumbe, akisisitiza umuhimu wa mshikamano miongoni mwa viongozi wa serikali za mitaa ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kusimamia maendeleo ya halmashauri kwa ufanisi. Kwa upande wake, Mhe. Tarimo alishukuru kwa imani aliyopewa na wajumbe wa ALAT, akiahidi kushirikiana na viongozi wote wa halmashauri katika mkoa wa Kilimanjaro kusukuma mbele ajenda za maendeleo, kuboresha utawala bora, na kuimarisha sauti ya serikali za mitaa katika ngazi za maamuzi. Uchaguzi huo unaashiria mwanzo wa awamu mpya ya uongozi wa ALAT mkoani Kilimanjaro, huku matarajio yakiwa ni kuona ushirikiano mkubwa zaidi kati ya halmashauri kwa maendeleo ya wananchi.