У нас вы можете посмотреть бесплатно DC MNZAVA ASHEREHEKEA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA RAIS DKT SAMIA KWA KUPANDA MITI MARINGENI SEKONDARI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mhe. Godfrey Mnzava amewataka wananchi kuzingatia sheria na taratibu za uvunaji wa miti kwa kuhakikisha wanapata vibali rasmi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kabla ya kufanya shughuli hiyo. Mhe. Mnzava ametoa kauli hiyo wakati wa zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Shule ya Sekondari Maringeni, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhamasisha upandaji miti nchini katika kuadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Amesema uvunaji holela wa miti umekuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira na kuchangia kasi ya mabadiliko ya tabianchi, hali inayohatarisha maisha ya sasa na ya vizazi vijavyo. Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito maalum kwa wakazi wa Kijiji cha Mande kilichopo Kata ya Old Moshi Magharibi kuendelea kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti na kulinda misitu iliyopo. “Utunzaji wa mazingira si hiari, ni wajibu wa kila mwananchi. Tukikata miti bila kupanda mingine tunajiandalia matatizo makubwa ya ukame na mmomonyoko wa udongo,” amesisitiza Mhe. Mnzava. Zoezi hilo la upandaji miti limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Katibu Tawala wa Wilaya ya Moshi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mwanga, watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, wawakilishi kutoka Taasisi ya Misitu Tanzania (TFS), wakazi wa Kijiji cha Mande pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maringeni. Hatua hiyo inaonekana kuwa sehemu ya juhudi zinazoendelea za serikali za kuhakikisha jamii inashiriki moja kwa moja katika vita dhidi ya uharibifu wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi.