У нас вы можете посмотреть бесплатно MITI 500 YAPANDWA TANGANYIKA, RAIS SAMIA APONGEZWA UTUNZAJI MAZINGIRA, DC BUSWELU AAGIZA HAYA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wananchi wa Wilaya ya Tanganyika wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la upandaji wa miti maarufu kama “27 ya Kijani”, lililoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni ishara ya kuunga mkono juhudi za kitaifa za utunzaji wa mazingira. Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Mhe. Onesmo Buswelu, na kufanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika, likiwakutanisha viongozi wa serikali, watumishi wa Halmashauri pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo. Ushiriki mkubwa wa wananchi umeonesha mwitikio chanya na uelewa wa jamii juu ya umuhimu wa kutunza mazingira. Katika zoezi hilo, zaidi ya miti 500 imepandwa katika maeneo ya hospitali na viunga vyake, kwa lengo la kuboresha mazingira, kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha afya ya jamii kwa ujumla. Kaulimbiu ya zoezi hilo ilikuwa “Uzalendo ni Kutunza Mazingira, Jitokeze Kupanda Miti.” Kaulimbiu hiyo ilihamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu katika upandaji na utunzaji wa miti kwa maendeleo endelevu ya Wilaya ya Tanganyika na taifa kwa ujumla.