У нас вы можете посмотреть бесплатно MAPYA YAIBUKA HIZI HAPA SABABU ZA G55 'KUMPINGA LISSU или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Msemaji wa kundi la wanachama wa Chadema la G55 linalokinzana na msimamo wa Chadema wa kutoshiriki uchaguzi iwapo hakutafanyika mabadiliko, John Mrema, ametaja sababu kuu tatu zinazowafanya kupinga mkondo huo wa chama, akisema hatua yao inalenga kulinda masilahi ya demokrasia na uhai wa chama chao. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumapili, Aprili 6, 2025, Mrema amesema sababu ya kwanza ni kukosekana kwa nafasi ya kutoa mawazo mbadala ndani ya chama, jambo ambalo linaathiri haki ya wanachama kujieleza na kushiriki kwenye maamuzi muhimu. Ametaja sababu ya pili kuwa ni ukosefu wa kauli thabiti kutoka kwa uongozi wa juu wa chama, hasa Mwenyekiti Tundu Lissu, katika kukemea kauli za baadhi ya makada wa Chadema wanaowashambulia wanachama wanaopinga msimamo wa kususia uchaguzi. Video na Ally Mlanzi