У нас вы можете посмотреть бесплатно KILIO CHA WAANDAMANAJI IRAN CHASIKIKA… или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwana wa kifalme wa Iran aliye uhamishoni Reza Pahlavi, ametoa wito mzito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono waandamanaji wanaopinga utawala wa Jamhuri ya Kiislamu, akiwa Marekani alisema ana imani kamili kwamba utawala wa sasa wa Iran utaanguka, akisisitiza kuwa si suala la kama bali ni lini jambo hilo litatokea. Pahlavi aliwataka viongozi wa dunia kuchukua hatua za moja kwa moja dhidi ya uongozi wa Kikosi cha walinzi wa Mapinduzi ya Iran, akisema hatua hiyo ingerahisisha mapambano ya waandamanaji na kupunguza upotevu wa maisha ya raia, kauli yake imekuja wakati Iran ikishuhudia maandamano makubwa yaliyotokana na hali mbaya ya uchumi na baadaye kubadilika kuwa madai ya kuondolewa kwa Kiongozi Mkuu, Ayatollah Ali Khamenei. BBC imeripoti kuwa, kwa mujibu wa makundi ya haki za binadamu, zaidi ya waandamanaji 2,600 wameuawa tangu maandamano yaanze mwishoni mwa Desemba, huku maelfu wengine wakikamatwa, serikali ya Iran, imekanusha madai hayo na kuyataja maandamano kama ghasia zinazoendeshwa na maadui wa taifa kutoka nje ya nchi. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Washington, Pahlavi alidai kuwa baadhi ya vyombo vya usalama vya Iran vimekataa kushiriki katika ukandamizaji wa waandamanaji, Aidha alidai kuwa serikali imewaleta wapiganaji kutoka makundi ya wanamgambo wa kigeni ili kusaidia kuzima maandamano yanayoendelea. Mbali na hilo, Pahlavi aliitaka dunia kuchukua hatua kali zaidi kama kuweka shinikizo la kiuchumi, kuwafukuza wanadiplomasia wa Iran, kudai kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa, na kusaidia upatikanaji wa mtandao kupitia teknolojia ya satelaiti kama Starlink ili kuvunja zuio la mawasiliano nchini humo. Alisisitiza kuwa watu wa Iran tayari wamechukua hatua madhubuti ndani ya nchi yao, na sasa ni jukumu la jumuiya ya kimataifa kusimama nao, kwa mujibu wake hata bila msaada wa dunia, utawala utaanguka, lakini msaada wa haraka unaweza kuokoa maisha mengi zaidi. Kauli za Pahlavi zimekuja sambamba na onyo la Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye aliwahi kuionya Iran dhidi ya kuua waandamanaji na kutishia kuchukua hatua kali, hata hivyo viongozi wa Iran wameonya kuwa shambulio lolote kutoka Marekani lingeifanya Israel pamoja na maslahi ya kijeshi ya Marekani katika eneo hilo kuwa malengo halali. Katika hatua ya tahadhari, Marekani na Uingereza zimepunguza idadi ya wafanyakazi wao katika kambi ya kijeshi ya Al-Udeid nchini Qatar, wakati huo huo Iran inaendelea na zuio la mtandao na ukandamizaji mkali, hali inayofanya upatikanaji wa taarifa za ndani ya nchi kuwa mgumu na kuongeza wasiwasi wa kimataifa kuhusu mustakabali wa taifa hilo.