У нас вы можете посмотреть бесплатно WATUHUMIWA 13 MBARANO KWA UTAPELI NA UNYANG'ANYI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja lilifanya Operesheni kuanzia tarehe 31 Januari 2026 ambapo katika Operesheni hiyo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 13 wanaohusika kwa wizi wa vifaa vya ujenzi kwa njia ya udanganyifu, Wahalifu wa Unyang'anyi kwa kutumia silaha na matapeli wa fedha. Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 03 Februari 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Thadei Mchomvu wakati akizungumza na vyombo vya habari huko ofisini kwake Madema. Amesema baadhi ya wezi hutumia namba za simu kuwapigia wauzaji wa vifaa vya ujenzi kama wateja na wanapofika eneo la ujenzi(site) huwatapeli wauzaji hao. Kamanda mchomvu amewataja watuhumiwa wanaohusika na wizi wa vifaa vya ujenzi kuwa ni (1) Ali Maulid Ali, miaka 29, MshirazI wa Mwanyanya (2) Salum Omary Abed, miaka 37, Mmakonde wa Mwanyanya (3) Abdallah Kombo Khamis, miaka 28, MshirazI wa Mwakaje, (4) Mudathir Said Khamis, miaka 22, MshirazI wa Mwanyanya, (5) Hamadi Iddi Mishim, miaka 35, MshirazI wa Bububu (6) Suleiman Idd Mishim, miaka 35, MshirazI wa Kama, Wote Wilaya ya Magharibi A" Hata hivyo ametoa wito kwa wamiliki wa maduka kuchukua tahadhari dhidi ya wezi hao na kuhakikisha wanalipwa kwanza kabla ya kufikisha mzigo kwenye eneo husika. Katika hatua nyingine Kamanda Mchomvu amesema Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa wengine sita (06) wanaounda kikundi cha kihalifu maarufu kama "Battery Low" ambao wanajihusisha na matukio mbalimbali ya kihalifu ikiwemo unyang'anyi kwa kutumia silaha na mashambulio ya kudhuru mwili. Watuhumiwa hao walifanya matukio yenye kuleta hofu kwa jamii na kujificha katika msitu wa Welezo uliopo Wilaya ya Magharibi A" Mkoa wa Mjini Magharibi. Upelelezi wa watuhumiwa hao unaendelea, hata hivyo juhudi za kumkamata kiongozi anaefadhili kikundi hicho zinaendelea. Sambamba na hayo Kamanda Mchomvu amebainisha kuibuka kwa kikundi cha kitapeli ambacho kilidai kuwakopesha fedha wananchi kwa sharti la kutoa asilimia 10% ya kiwango cha mkopo unaoombwa. Kikundi hicho kilichoongozwa na wananchi watatu (03) kilikusanya fedha takriban Milioni saba (7,000,000) kutoka kwa wananchi 15 kisha kutoweka na fedha hizo. Watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa mahojiano. Akizungumza kuhusu uwepo wa ajali za usalama barabarani Kamanda Mchomvu amesema kumekuwa na ajali zinazotokana na uzembe wa baadhi ya madereva kutozingatia sheria za usalama barabarani jambo ambalo linapelekea ajali zinazogharimu maisha ya watu na hata ulemavu. Katika kuzuia na kupambana na ajali hizo, Kamanda Mchomvu amesema Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limeanzisha Doria za barabara kuu (Highway Patrol) ili kuhakikisha kila dereva anatii sheria na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya dereva atakaenda kinyume na sheria hizo.