У нас вы можете посмотреть бесплатно DC LUDEWA AOMBA RIDHAA YA EKARI 120 KUJENGA UWANJA WA NDEGE MAWENGI NA MBWILA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
WANANCHI MAWENGI NA MBWILA WARIDHIA KUTOA ZAIDI YA EKARI 120 KUJENGA UWANJA WA NDEGE Wananchi wa Kijiji cha Mawengi (Kata ya Mawengi) na Kijiji cha Mbwila (Kata ya Luana), wilayani Ludewa, kwa kauli moja wameridhia kutoa zaidi ya ekari 120 za ardhi kwa kampuni ya uwekezaji ya HWTZ kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja cha ndege. Makubaliano hayo yamefikiwa katika mikutano mikubwa ya hadhara iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Olivanus Thomas, aliyefika vijijini humo kuutambulisha mradi na kuomba ridhaa ya wananchi kama wamiliki halali wa ardhi. Akizungumza kwenye mikutano hiyo, Mkuu wa Wilaya alisema ujenzi wa kiwanja cha ndege ni sehemu ya uwekezaji mkubwa wa HWTZ, ikiwemo ujenzi wa Kiwanda cha Saruji Masimbwe, uchakataji wa chuma na madini ya titanium pamoja na utengenezaji wa vifaa mbalimbali, hali itakayozifanya maeneo hayo kuwa kongani ya viwanda. Alifafanua kuwa uwekezaji huo utahusisha pia vijiji vya Mdilili kwa uchimbaji wa chuma, Lupanga (eneo la Nyaluva) kwa uchimbaji wa chuma, na Muhumbi kwa uchimbaji wa makaa ya mawe yatakayozalisha umeme kwa ajili ya kuendesha viwanda hivyo. Mkuu huyo wa Wilaya alisema changamoto kubwa iliyopo ni miundombinu ya usafiri, hivyo wawekezaji wameamua kujenga uwanja wa ndege utakaorahisisha shughuli za uzalishaji na usafirishaji. Uwanja huo utajengwa katika eneo linalopakana kati ya Kitongoji cha Newele (Kijiji cha Mawengi) na Kitongoji cha Magomeni (Kijiji cha Mbwila). Alisisitiza kuwa wananchi wote watakaoguswa na mradi watalipwa fidia kwa mujibu wa sheria na taratibu zote za kiserikali. Kwa upande wao, wananchi wa Mawengi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji, Humphrey Atanasio, pamoja na wananchi wa Mbwila wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Frank Haule, wamekubali kutoa ardhi hiyo na kuonesha furaha yao wakisema uwanja wa ndege utaleta fursa za ajira na maendeleo ya kiuchumi. Mikutano hiyo ilihudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Castor Kibasa, wataalamu wa halmashauri, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Joseph Kamonga