У нас вы можете посмотреть бесплатно RC MALIMA AWATEMBELEA MAJERUHI AJALI MOROGORO, ALIA NA MADEREVA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, amewatembelea na kuwapa pole majeruhi wa ajali ya basi la abiria lililokuwa likifanya safari yake kutoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam, baada ya kugongana uso kwa uso na lori la mizigo. Ajali hiyo ambayo imetokea alfajiri ya leo Juni 11, 2025 imesababisha vifo vya watu tisa papo hapo na mmoja kufariki dunia akiwa njiani akipelekwa hospitalini kupatiwa matibabu, hivyo kufanya jumla ya vifo kufikia kumi na majeruhi 45. Ajali hiyo imetokea eneo la Lugono Wilayani Mvomero, mkoani Morogoro huku Mkuu huyo wa mkoa amewatembelea majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kuwapa pole kwa kadhia hiyo iliyowakuta. Hata hivyo Mhe. Malima amesema uwekezaji mkubwa uliowekezwa na Serikali ya awamu ya sita katika sekta ya Afya ndiyo inayosaidia kutopoteza majeruhi wengi wanaopelekwa hospitalini hapo kwa sababu ya ubora wa vitendea kazi na watoa huduma wake. "Watoto wote wanaendelea vizuri. Tumeenda kuwaona hivi sasa, wana maumivu makubwa lakini hali zao zinaendelea kuimarika...” amesema Mhe. Adam Malima Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo Mhe. Malima amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali zinazotokana na uzembe, ikiwa ni pamoja na kuendesha bila kuchoka na kuheshimu muda wa mapumziko. Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Daniel Nkungu, amethibitisha kupokea miili ya watu kumi na majeruhi 45, wakiwemo wanawake, wanaume na watoto. Kati ya miili hiyo, sita tayari imetambuliwa na ndugu zao huku juhudi zikiendelea kufanikisha utambuzi wa miili iliyobaki. Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta dereva wa gari aina ya Scania lenye namba za usajili T.404 CZS, ambalo lilikuwa limebeba shehena ya sukari na ndilo linalodaiwa kusababisha ajali hiyo. MWISHO