У нас вы можете посмотреть бесплатно Rais Samia akerwa na matukio ya utekaji na mauaji, awapa machifu kibarua kukomesha или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka machifu nchini kukemea vitendo vya utekaji na mmomonyoko wa maadili vinavyoendelea katika maeneo mbalimbali nchini. Amesema hayo leo Jumamosi Julai 20,2024 alipokutana na kuongea na machifu nchini, hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Dodoma. Kauli hiyo ya Rais inakuja wakati Mwananchi likiwa limeripoti habari za watu wanaodaiwa kutekwa, ikiwamo tukio la mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam Edgar Mwakabela ‘Sativa’ aliyetoweka Juni 23, 2024 na kupatikana Juni 27 katika Pori la Hifadhi ya Katavi akiwa na majeraha mwilini. Ukiacha suala la Sativa tukio jingine ni la Kombo Mbwana kada wa Chadema wilayani Handeni mkoani Tanga, aliyetoweka tangu Juni 15 na wiki iliyopita ilibainika kuwa alikuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi. Kutokana na kelele za wanaharakati na wanasheria mbalimbali, zimewezesha Kombo kufikishwa mahakamani. Hata hivyo, Julai 3 2024 Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni alisema Tanzania iko salama na vitendo vya utekaji havipaswi kukaliwa kimya, akirejea chapisho la Mwananchi la Julai 2,2024 lililokuwa na kichwa cha habari: Nani mtekaji? Akizungumza leo kuhusu matukio hayo ya utekaji, Rais Samia amesema anashangaa kuona vitendo hivyo vya utekaji vikishamiri kila kukicha lakini viongozi hao wakiwa kimya na kutokemea.