У нас вы можете посмотреть бесплатно VIKUNDI 308 KUNEEMEKA NA BILIONI 3.6 ZA MIKOPO YA 10% DODOMA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Benki washirika (NMB na CRDB) wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika utoaji mikopo ya 10% ya mapato ya ndani, wametakiwa kuhakikisha wanakamilisha hatua zao kwa wakati na uharaka ili iwafikie walengwa kwa muda uliopangwa. Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa hafla ya uzinduzi wa utoaji mikopo ya 10% kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, iliyofanyika Agosti 28, 2025 katika viwanja vya 'Nyerere Square' jijini Dodoma. "Benki zote mbili, nyie ni washirika katika utoaji wa mikopo hii, pamoja na vigezo mnavyovisimamia naomba muwe msaada mkubwa kwa wananchi hawa wapate mikopo hii kwa haraka, ni kiu yao kuona ahadi aliyotoa Rais wao inawafikia kwa wakati," amesema Senyamule. Pia Mhe. Senyamule ametumia fursa hiyo kuwaasa wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia vyema na kuepukana na mkono wa sheria pindi watakapokwenda kinyume na mikataba yao. "Napenda kuwakumbusha kuwa mikopo hii siyo zawadi bali ni mikopo nafuu isiyo na riba, ni vema mkaitumia vizuri na kuirejesha kwa wakati kama mlivyosaini mikataba yenu ili na wengine waweze kunufaika na fursa hii. Binafsi nisingependa kuona mwanakikundi yeyote anafikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kushindwa au kukwepa kurejesha mkopo," ameongeza Senyamule. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amesema wilaya yake ipo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha jambo hilo. "Niwaombe wadau ambao mtapewa mikopo hii leo, mkawe mabalozi wazuri, mkatumie fedha vizuri, mkafanye marejesho kwa wakati ili muwaondoshe hofu mabenki. Hizi changamoto za leseni ya biashara sisi tupo tayari kuwa na timu ya pamoja na watu wa halmashauri ili wakija ambao hawana washughulikiwe kwa haraka na wapatiwe mkopo wasikwame," amesema Shekimweri. Akitoa taarifa za mikopo hiyo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Fredrick Sagamiko amesema Bilioni 3,617,857,852.00 zitakopeshwa kwa vikundi 308 kupitia benki za NMB na CRDB. Fedha hizo zimekusanywa kupitia mapato ya ndani kwa miaka miwili, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Tanzania kuwa halmashauri zote Nchini zitenge 10% ya mapato yao na kuzikopesha bila riba kupitia vikundi vya uzalishaji vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu. Hata hivyo Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na VETA Dodoma wameandaa mafunzo kwa vijana watakaonufaika na mikopo ya bajaji na bodaboda, ili kukidhi vigezo vya kuendesha vyombo hivyo ikiwemo kuwa na leseni za udereva. Mafunzo hayo yatatolewa kwa gharama nafuu na yanatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Septemba.