У нас вы можете посмотреть бесплатно TAZAMA WAZIRI JAFO ALIVYOTOA MAAGIZO HAYA JUU YA ATHARI ZA KELELE KWA AFYA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
ATHARI ZA KELELE KWA AFYA:JAFO ATOA SIKU 7 ZA KUJIREKEBISHA WAMILIKI WA KUMBI ZA STAREHE Kutokana na kukithiri Kwa uchafuzi wa Mazingira unaotokana na kelele na mitetemo, Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mheshimiwa Seleman Jafo ametoa siku saba (7) kwa wamiliki wa maeneo yote yanayofanya uchafuzi huo kurekebisha utoaji wa huduma zao ili ziendane na takwa la sheria ya mazingira na kanuni zake. Jafo ametoa agizo hilo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuagiza baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC kufungia maeneo yote yatakayokaidi kutekeleza sheria na kanuni za Mazingira kuhusu kelele na mitetemo. Waziri Jafo amesema sheria ya Mazingira ya 191 Kifungu cha 106 Kifungu kidogo cha (5 na 6) kinakataza kupiga kelele kuzidi viwango vinavyoruhusiwa na vilevile ni kosa kupiga kelele kinyume na viwango vilivyoruhusiwa hali ambayo huhatarisha afya za binadamu. Aidha kanuni za udhibiti wa kelele na mitetemo za mwaka 2015 zimeainisha viwango vya sauti vinavyoruhusiwa kwenye maeneo ya makazi,Biashara, Viwanda na Hospitali ili kulinda afya ya jamii. Jafo amesema hatua za kisheria zilizoainishwa kwenye sheria ni pamoja na kutozwa faini na kufungiwa biashara kwenye maeneo yaliyokithiri kwa kelele na mitetemo. Amesema pamoja na kuchukua hatua hizo za kisheria kumekua na ongezeko la malalamiko ya kelele na mitetemo kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 ambapo asilimia 65 ya malalamiko yaliyowasilishwa na baraza la mazingira yanahusu kelele na mitetemo hali inayoonyesha adhabu za kutozwa faini hazitoshi kwa wanaokamatwa. #elimuyaafyakwaumma Pata elimu kuhusu masuala yote ya afya kupitia Channel hii. Mafunzo yote yanatolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara ya Kinga, Kitengo Cha Elimu ya Afya kwa Umma kwa kushirikiana na wadau mbali mbali #elimuyaafyakwaumma