У нас вы можете посмотреть бесплатно TEMESA YAKAMILISHA MATENGENEZO KIVUKO MV. KILAMBO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bi. Bahati Geuzye, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha TEMESA kukifanyia matengenezo kivuko cha MV. KILAMBO kilichokuwa kinasaidia kutoa huduma eneo la Lindi – Kitunda mara baada ya kivuko MV. KITUNDA kinachotoa huduma eneo hilo kuondolewa kwenye maji kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati mkubwa. Akizungumza na vyombo vya Habari leo tarehe 09 Agosti 2023, Bi.Geuzye ambaye aliongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mtwara, amesema kuwa wamefika eneo hilo kwa ajili ya kukagua matengenezo yaliyofanyika kwenye kivuko hiko ambapo pia amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa kuwapa ridhaa ya kufanya ukaguzi kwenye kivuko hiko. Bi. Geuzye amesema wametembelea kukagua na wameona namna TEMESA imefanya matengenezo makubwa hasa kwenye upande wa injini, kurekebisha vipuri mbalimbali na kukiboresha kivuko hiko na kuwahakikishia wananchi kuwa hivi karibuni kitaenda kutoa huduma mpakani mwa Mtwara eneo la Kilambo na Namoto.