У нас вы можете посмотреть бесплатно 🔴 WAPIGA KURA 120,780 KISHIRIKI ZOEZI LA KUMCHAGUA MBUNGE JIMBO LA PERAMIHO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Msimamizi wa Uchaguzi Mdogo katika Jimbo la Peramiho, Evavery Luyagaza, amesema jumla ya wapiga kura 120,780 wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari 26, 2026, huku jumla ya vituo vya kupigia kura vikiwa 354. Akizungumza kuhusu maandalizi ya uchaguzi, Luyagaza amesema kampeni zinatarajiwa kutamatika Februari 25, 2026, siku moja kabla ya wananchi kuelekea kupiga kura. Amebainisha kuwa hadi sasa kampeni za vyama vya siasa zinaendelea vizuri bila changamoto yoyote kubwa iliyoripotiwa. Kuhusu elimu ya mpiga kura, amesema ofisi yake imejipanga kuanza kutoa elimu kupitia redio za ndani pamoja na matangazo ya kutembea katika kila kitongoji, kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo muhimu la kidemokrasia. Aidha, ameeleza kuwa maandalizi mbalimbali yanaendelea kuhakikisha uchaguzi unafanyika bila vikwazo vyovyote. Hatua hizo ni pamoja na uandaaji wa vituo vya kupigia kura na ubandikaji wa matangazo yenye taarifa muhimu kwa wapiga kura. Luyagaza ametoa wito kwa wananchi wa Jimbo la Peramiho kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemtaka.