У нас вы можете посмотреть бесплатно NAIBU WAZIRI CHUMI APOKEA MSAADA WA TENDE TANI 75 KUTOKA SAUDI ARABIA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) amepokea msaada wa tende tani sabini na tano (75) kutoka kwa serikali ya Saudi Arabia, katika hafla iliyofanyika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam Februari 19, 2025. Mhe. Chumi amesema msaada huo umekuja katika kipindi muafaka kwani ni kipindi ambacho tunaelekea kwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na kuongeza kuwa katika msada huo wa tani 75, tani 50 zitagawanywa Tanzania Bara na tani 25 zitagawiwa Visiwani Zanzibar. Aidha Mhe. Naibu Waziri Chumi ameongeza kuwa Saudi Arabia imekuwa mshirika na rafiki mkubwa wa Tanzania kwani ukiachilia mbali msaada huu wa tende, yapo mengi ambayo yanafanywa na Saudi Arabia hapa nchini, kama vile mwaka jana 2024 ilikuja timu ya wataalam wa afya na kutoa matibabu bure kwa watoto zaidi ya watoto 70 na wengine 25 kutoka familia za kawaida kufanyiwa upasuaji wa moyo kwenye kituo cha Magonjwa ya Moyo JKCI, huku mwezi mei mwaka huu 2025 wakitarajiwa kuwasili Madaktari na Wataalamu wengine kwaajili ya kuendelea kutoa msaada wa matibabu. Msaada huo umewasilishwa na Balozi wa Saudi Arabia hapa nchini Mhe. Yahya Al Okeish, kwa niaba ya Mfalme wa Saudi Arabia Mhe. Salman bin Abdulaziz Al Saud. Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Mhe. Balozi Okeish amesema siku zote serikali ya Saudi Arabia imekuwa mstari wa mbele kutoa misaada mbalimbali kwa nchi mbalimbali zenye uhitaji duniani kote, huku akiishukuru serikali ya Tanzania kwa jinsi ambavyo wamefanikisha kupokelewa kwa msaada huu.